
๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
February 12, 2025 at 07:37 AM
USIJITOLEE KUPITA KIASI KATIKA MAHUSIANO
*Mapenzi ni kitu kizuri ndio, lakini mara nyingi huwatokea watu puani kwa sababu ya kujitoa kupita kiasi kwa mtu asiye na nia nzuri katika mahusiano hayo. Unapompenda mtu, ni kawaida kutaka kumpa kila kitu, muda wako, hisia zako, na hata kujinyima kwa ajili yake. Lakini je, unahakikisha kuwa yeye anathamini hilo?*
Usijitolee kupita kiasi kwa mtu ambaye hajathibitisha kuwa anakuheshimu na kukuthamini. *Mahusiano mazuri ni yale yanayoenda kwa uwiano, si pale ambapo mmoja anajitoa kupita kiasi na mwingine hana mpango na hayo mahusiano.*
Kama wewe kila mara ndiye unayetuma ujumbe kila wakati, unayejali, unayejitahidi kumfurahisha, huku mwenzako hana juhudi zozote, jua kwamba kuna tatizo. *_Upendo wa kweli haukufanyi uhisi kuwa unalazimika kudhihirisha thamani yako kwa kujitolea kupita kiasi._*
Mtu anayekupenda kweli hatakufanya uhisi kwamba unatakiwa kujipoteza ili umpate. Atakuheshimu, atajali hisia zako, na atafanya juhudi kama unavyofanya.
*Jifunze kupenda bila kujidhalilisha.*
Kama unajitoa kupita kiasi na huoni juhudi kutoka upande wa pili, punguza mwendo, jithamini, na ujue kuwa unastahili kupendwa kwa dhati bila masharti.
WhatsApp In-box ๐ https://wa.me/message/36OZ47M2H4RAA1
WhatsApp Channel OTHUMAN FACT Channel. ..https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s

โค๏ธ
๐
๐ค
3