๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
February 14, 2025 at 02:21 PM
Kuna msimu unafika, kila mtu anataka kuonekana yuko kwenye mahaba mazito. *_Miji inajaa maua, mapambo mekundu kila kona, simu zinapokea jumbe tamu za mapenzi, na mitandao inashamiri picha za watu waliopokea zawadi._* Ukiangalia huku na kule, unahisi kana kwamba dunia yote ina mapenzi mazito isipokuwa wewe. *Lakini je, huu ni wakati wa kupoteza mwelekeo kwa sababu ya msimu wa mapenzi?* Ni kweli thamani yako Unapaswa kuipima kwa maua, chocolates, au dinner za usiku wa Valentine? *Mapenzi ya kweli hayapimwi kwa siku au Usiku mmoja wa sherehe.* Mapenzi ya kweli yapo kwenye mambo madogo yanayofanyika kila siku, kujali, kuheshimiana, na kuwa na mtu ambaye anakuthamini bila kujali tarehe, siku Wala mwaka. *Usikubali shinikizo la msimu likufanye ujione dhaifu au kukuharakisha kufanya maamuzi ambayo baadaye utajutia Kwa maisha yako yote.* Usikubali kuingia kwenye uhusiano kwa sababu tu marafiki zako wamejawa na zawadi. *Usiukubali mwaliko usio na mipango kwa sababu ya hofu ya kuwa peke yako.* *Kumbuka,* mapenzi ya kweli hayatokei kwa presha, yanatokea kwa wakati sahihi, kwa mtu sahihi, na kwa sababu sahihi. Kama kuna mtu anakupenda kweli, ataonesha upendo wake si kwa shinikizo la _tarehe 14 Februari pekee,_ bali kwa vitendo vyake vya kila siku. Na kama hujapata mtu wa kweli, ni bora kubaki peke yako kwa amani kuliko kuingia kwenye matatizo yasiyo na mwisho kwa ajili ya sherehe ya siku moja. *Usiruhusu mapenzi ya msimu yakuingize kwenye adhabu ya maisha.* Itambue thamani yako, tuliza moyo wako, na subiri kile chenye maana ya kweli!. WhatsApp In-box ..https://wa.me/message/36OZ47M2H4RAA1 WhatsApp Channel OTHUMAN FACT Channel. ..https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s
Image from ๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง: Kuna msimu unafika, kila mtu anataka kuonekana yuko kwenye mahaba mazi...
๐Ÿ”ฅ ๐Ÿ˜ข ๐Ÿ™ 3

Comments