๐ข๐ง๐๐จ๐ ๐๐ก ๐๐๐๐ง
February 16, 2025 at 11:05 AM
Ni Ukweli kwamba Kupenda/kupendwa ni kitu kizuri sana, lakini mapenzi peke yake hayawezi kuwa ndo msingi wa maisha yako yote.
*Watu wengi wanaweka mapenzi katikati ya kila kitu kwenye maisha yao, kiasi kwamba wanapoumizwa, wanapoteza mwelekeo kabisa wa maisha.*
Jifunze kuwa na maisha nje ya mahusiano. Kuwa na malengo yako, ndoto zako, marafiki zako, na mambo yanayokuletea furaha hata bila uhusiano wa kimapenzi.
*Mtu kama kweli anakupenda kwa dhati anataka kuona unafanikiwa katika maisha yako binafsi, si tu kwa kuwa tegemezi kwake kwa kila kitu cha kihisia, na maisha.*
Ukifanya mapenzi kuwa kila kitu, utaumia zaidi pale mambo yasipoenda kama ulivyotarajia.
*Lakini ukiyachukulia kama sehemu tu ya maisha, utaweza kupenda bila kupoteza utambulisho wako.*
Mapenzi yanapaswa kuwa nyongeza ya furaha uliyonayo, na si chanzo pekee cha furaha yako. *Mapenzi Si Kila Kitu.*
WhatsApp In-box ๐ https://wa.me/message/36OZ47M2H4RAA1
WhatsApp Channel OTHUMAN FACT Channel. ..https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s
โค๏ธ
๐
2