๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง
February 22, 2025 at 10:05 AM
*ACHA KUJICHUNGUZA SANA, ANZA KUTHUBUTU SASA!* Mara nyingi ndoto kubwa zinaanza kufifia pale mtu anapoanza kujichunguza kupita kiasi. Kila anapojaribu kupiga hatua, sauti yake ya ndani inamwambia, "Je, nitaweza? Mimi si wa kiwango hicho. Sijui kama nina uwezo wa kutosha. Watu watasema nini?" *Huu ni mtego hatari unaozimaliza ndoto za watu wengi hata kabla ya kuanza.* Kasome kisa Cha *_Musa alipopokea wito wa kwenda kwa Firauni, hakuhisi kama yuko tayari. Akasema, "Mola wangu! Mimi naogopa kuwa watanikanusha, na kifua changu kinabanwa, na ulimi wangu haufunguki vizuri." Kasome Quran ..Surah (Ash-Shu'ara 26:10-13)._* *_Lakini pamoja na hofu zake, bado Mwenyezi Mungu alimpa msaada wa Harun na akamsimamisha kwa kazi hiyo kubwa._* Inamaanisha nini hii kwamba kila mtu anayeota mambo makubwa lakini anajiwekea mipaka kwa sababu ya hofu na mashaka binafsi. *Haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani, kama utajipa muda wa kujichunguza sana, lazima utaona kasoro na sababu za kushindwa hata kama hazipo.* Ulimwengu haujengwi na watu waliokamilika, bali na watu waliothubutu. Watu waliokataa kusikiliza sauti za hofu na wakaamua kuchukua hatua hata wakiwa na mashaka. Usiruhusu tabia ya kujichunguza sana ikufanye uhisi hauna neema ya kufanya mambo makubwa. *Chukua Hatua, Anguka, Simama Tena, Jifunze, Songa Mbele.* Ndoto yako haihitaji ukamilifu inahitajika tu hatua yako ya kwanza! Ili kuendelea mbele. WhatsApp In-box ..https://wa.me/message/36OZ47M2H4RAA1 WhatsApp Channel OTHUMAN FACT Channel. ..https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s
Image from ๐—ข๐—ง๐—›๐—จ๐— ๐—”๐—ก ๐—™๐—”๐—–๐—ง: *ACHA KUJICHUNGUZA SANA, ANZA KUTHUBUTU SASA!*  Mara nyingi ndoto kubw...
โค๏ธ ๐Ÿ‘ ๐Ÿ™ 3

Comments