Nukta Habari
Nukta Habari
February 7, 2025 at 12:28 PM
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), sonona ni hali ya kiakili inayoathiri hisia na uwezo wa mtu kufanya kazi za kila siku ikikadiriwa kuathiri watu zaidi ya milioni 280 duniani kote huku zaidi ya asilimia 50 wakiwa ni wanawake. Pamoja na takwimu hizo WHO inabainisha kuwa asilimia 10 ya wanawake wajawazito duniani na asilimia 13 ya wale waliojifungua hukutana na tatizo hilo. “Katika nchi zinazoendelea, hali hii ( sonona) ni ya juu zaidi kwa asilimia 15.6 wakati wa ujauzito na asilimia 19.8 baada ya kujifungua. Matatizo haya yanaweza kuwa makubwa akiasi cha kusababisha mama kujiua,” imesema WHO. Evarista Jacob ni miongoni mwa wanawake waliokutana na tatizo la sonona lilioanzia wakati wa ujauzito na baadae kuendelea kumuathiri alipojifungua mtoto wake wa kwanza. https://nukta.co.tz/jinsi-ya-kukabiliana-na-sonona-kabla-na-baada-ya-kujifungua
Image from Nukta Habari: Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), sonona ni hali ya kiakili...

Comments