
Nukta Habari
46 subscribers
About Nukta Habari
A product of Nukta Africa
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Serikali ya Tanzania imepanga kukuza na kulinda viwanda vya ndani baada ya kupendekeza maboresho mengi ya kodi, tozo na ushuru wa forodha wa bidhaa katika bajeti ya mwaka 2025/26. Hatua hizo ni mwendelezo wa Serikali kukuza sekta ya viwanda ambayo ni moja ya vichocheo vikubwa vya ukuaji wa uchumi kwa kutoa ajira na kuzalisha bidhaa zinazopunguza matumizi ya bidhaa kutoka nje ya nchi. https://nukta.co.tz/namna-tanzania-inavyotaka-kulinda-viwanda-vya-ndani-bajeti-2025-26

Licha ya Serikali kuongeza bajeti ya sekta ya kilimo wabunge wameelezea wasiwasi wao kuhusu ufanisi wa uwekezaji huo, wakitaka mabadiliko ya dhati yatakayoongeza tija, ushindani na masoko ya uhakika kwa wakulima. Sekta ya kilimo inaongoza kwa kuchangia kiwango kikubwa cha pato la taifa (GDP) ikichangia kwa asilimia 26 ya Sh156 trilioni zilizoripotiwa mwaka 2024, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Mipango na Uwekezaji. https://nukta.co.tz/wabunge-walia-bajeti-ya-kilimo-wakitaka-mageuzi

Tumia viwango hivi leo kubadili fedha za kigeni dhidi ya shilingi ya Tanzania


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Wambura, amefanya mabadiliko ya uongozi kwa kuwahamisha makamanda watatu wa polisi katika mikoa na vitengo mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya kawaida ndani ya jeshi hilo. Kwa mujibu wa taarifa iloiyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime leo Juni 17, 2025 imeeleza kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID) yaliyopo jijini Dodoma. https://nukta.co.tz/igp-wambura-apangua-makamanda-wa-polisi

Mwenyekiti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu amepewa ruhusa na mahakama kujitetea mwenyewe katika kesi ya uhaini badala ya mawakili wake kwa madai ya kuwa wamenyimwa fursa ya faragha kuongea naye. Ombi hilo lililokubaliwa na mahakama leo Jumatatu Juni 16, 2025 litamfanya Lissu kuchuana na mawakili wa Serikali katika kesi hiyo inayofuatiliwa kwa karibu na wadau wa haki za binadamu ndani na nje ya nchi. https://nukta.co.tz/lissu-kujitetea-mahakamani-kesi-ikipigwa-kalenda

Huenda matumizi ya nishati safi ya kupikia yakapata msukumo mpya nchini Tanzania mara baada ya Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuzindua kampeni mpya ya Pika Smart inayolenga kuhamasisha matumizi ya kupika kwa kutumia nishati ya umeme. Kampeni ya Pika Smart ni sehemu ya juhudi za kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini ili kufikia lengo la asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. https://nukta.co.tz/serikali-wadau-wa-maendeleo-wazindua-kampeni-ya-pika-smart

Tumia viwango hivi kubadili fedha za kigeni dhidi ya shilingi ya Tanzania
