Tanzanian Catholics Online
Tanzanian Catholics Online
February 9, 2025 at 02:57 PM
WITO NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema wametakiwa kupokea wito ambao wanaitiwa na Mwenyezi Mungu kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Hayo yameelezwa na Padre John Mbivilila, Paroko wa Parokia Teule ya Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe Mwilamvya Jimbo Katoliki Kigoma, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu Dominika ya 5 ya mwaka C wa Kanisa iliyoadhimishwa Parokiani hapo. Amewataka waamini kutokuwa na kigugumizi katika kuitikia sauti ya wito kama vile ndoa, upadre, utawa na miito mingine inayopatikana katika Kanisa na jamii kwa ujumla. Aidha, amesema kila mtu anapaswa kuonja uwepo na upendo wa Mungu katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na kutimiza mapenzi ya Mungu kwa kadiri ya miito mbalimbali ambayo wanadamu wanaitwa kuitumikia. Padre Mbivilila, amewasisitiza zaidi Wakristo kuacha tabia ya kukwepa kumtumikia Mungu kwa visingizio mbalimbali ambavyo vinawafanya watu watu wengi kujitenga na mwenyezi Mungu, badala yake wanapaswa kumtumikia kwa karama na vipawa vyao ambavyo wamepewa na Mwenyezi Mungu. Vile vile amewahimiza waamini kutoka kata tamaa katika changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kuitikia wito wa kumtumikia Mungu, badala yake wanatakiwa kusali na kumuomba Mungu ili awatie nguvu zaidi ya kuitikia sauti ya wito wa Mungu. Padre Mbivilila, amehitimisha homilia kwa kuwataka watu kuwa na tabia ya kuomba msamaha kwa Mungu na wanadamu pale wanapokuwa wanakosea, ilikuendelea kuimarika zaidi na kupata nguvu zaidi katika kumtumikia Mungu. Na Samwel Wambura Radio Maria Tanzania - Kigoma www.radiomaria.co.tz #radiomariatz #mahujajikatikamatumaini #injilishakwaharaka
Image from Tanzanian Catholics Online: WITO NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU  Wakristo na watu wote wenye mapenzi m...
🙏 1

Comments