Tanzanian Catholics Online WhatsApp Channel

Tanzanian Catholics Online

147 subscribers

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

Tanzanian Catholics Online
Tanzanian Catholics Online
2/2/2025, 12:34:05 AM

*MASOMO YA MISA TAKATIFU , DOMINIKA YA SIKUKUU YA KUTOLEWA YESU HEKALUNI* *SOMO 1: Mal 3:1-4* Bwana Mungu asema hivi: Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki. Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani. *WIMBO WA KATIKATI Zab 24:7-10* Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. (K) Ni nani mfalme wa utukufu! Ni Bwana, mwenye nguvu, hodari Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita. (K) Ni nani mfalme wa utukufu! Ni Bwana, mwenye nguvu, hodari Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. (K) Ni nani mfalme wa utukufu! Ni Bwana, mwenye nguvu, hodari Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu. (K) Ni nani mfalme wa utukufu! Ni Bwana, mwenye nguvu, hodari *SOMO 2: Ebr 2:14-18* Kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa. *SHANGILIO: LK 2:32* Aleluya, aleluya! Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli. Aleluya! *INJILI: Lk 2:22-40* Zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana, (kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana), wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili. Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, Uliouweka tayari machoni pa watu wote; Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli. Na babaye na mamaye walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake. Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi. Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake. Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti. Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Nakutakia Dominika Njema ...🙏

Image
Tanzanian Catholics Online
Tanzanian Catholics Online
2/9/2025, 2:57:38 PM

WITO NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema wametakiwa kupokea wito ambao wanaitiwa na Mwenyezi Mungu kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Hayo yameelezwa na Padre John Mbivilila, Paroko wa Parokia Teule ya Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe Mwilamvya Jimbo Katoliki Kigoma, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu Dominika ya 5 ya mwaka C wa Kanisa iliyoadhimishwa Parokiani hapo. Amewataka waamini kutokuwa na kigugumizi katika kuitikia sauti ya wito kama vile ndoa, upadre, utawa na miito mingine inayopatikana katika Kanisa na jamii kwa ujumla. Aidha, amesema kila mtu anapaswa kuonja uwepo na upendo wa Mungu katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na kutimiza mapenzi ya Mungu kwa kadiri ya miito mbalimbali ambayo wanadamu wanaitwa kuitumikia. Padre Mbivilila, amewasisitiza zaidi Wakristo kuacha tabia ya kukwepa kumtumikia Mungu kwa visingizio mbalimbali ambavyo vinawafanya watu watu wengi kujitenga na mwenyezi Mungu, badala yake wanapaswa kumtumikia kwa karama na vipawa vyao ambavyo wamepewa na Mwenyezi Mungu. Vile vile amewahimiza waamini kutoka kata tamaa katika changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kuitikia wito wa kumtumikia Mungu, badala yake wanatakiwa kusali na kumuomba Mungu ili awatie nguvu zaidi ya kuitikia sauti ya wito wa Mungu. Padre Mbivilila, amehitimisha homilia kwa kuwataka watu kuwa na tabia ya kuomba msamaha kwa Mungu na wanadamu pale wanapokuwa wanakosea, ilikuendelea kuimarika zaidi na kupata nguvu zaidi katika kumtumikia Mungu. Na Samwel Wambura Radio Maria Tanzania - Kigoma www.radiomaria.co.tz #RadiomariaTz #Mahujajikatikamatumaini #Injilishakwaharaka

Post image
🙏 1
Image
Tanzanian Catholics Online
Tanzanian Catholics Online
2/17/2025, 6:10:54 AM

https://youtu.be/hMuaVVEmN3U?si=xvzbFvcd1n4nt56M Usiahau ku-SUBSCRIBE kupitia link hii https://youtube.com/@asalimubashara?si=x-OFlyZwW6PI8G4z watumie pia wengine waweze kulisikia neno la Mungu na kulishika. MASOMO YA MISA, FEBRUARI 17, 2025 JUMATATU, JUMA LA 6 LA MWAKA Mwa 4: 1-15, 25; Adamu alimjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyma dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Kaini akamwambia Habili nduguye, twende uwandani. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua. Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoto na mtu asiye na kikao duniani. Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami niakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pia Habili; kwa sababu Kaini alimwua. Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu. WIMBO WA KATIKATI Zab. 50:1, 8, 16 – 17, 20 – 21 (K) 14 (K) Umtolee Mungu dhabihu za kushukuru. Mungu, Mungu Bwana, amenena, ameiita nchi, Toka maawio ya jua hata machweo yake. Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele zangu daima. (K) Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako? Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. (K) Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia. Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza, Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako. (K) SHANGILIO 1Sam. 3:9 Aleluya, aleluya, Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia: Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Aleluya. INJILI Mk. 8:11 – 13 Walitokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana na Yesu; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu. Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki. Akawaacha akapanda tena chomboni, akaenda zake hata ng’ambo. Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo. *ASALI MUBASHARA-Jumatatu 17/02/2025* Karibuni ndugu zangu wapendwa kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana linaanza kwa kuiangalia Zaburi yetu ya Wimbo wa katikati toka zaburi ya 50. Hapa tunakutana na Zaburi isemayo: umtolee Mungu dhabihu za kushukuru. Hii ni amri, zaburi hii inasisitiza pia tena kwamba kila tujapo kwa Bwana kwa ajili ya hii dhabihu, lazima moyo wetu uwe safi. Na hapa Bwana huipokea na kuibariki dhabihu hii. Leo katika masomo yetu, anayetimiza hili ni Abeli. Yeye anakuja mbele ya Bwana na dhabihu ya kushukuru, na anakwenda na moyo safi, na dhabihu yake inakubaliwa. Kaini anakwenda na moyo mkaidi, na mara moja inakataliwa. Moyo wa uchoyo na hasira na chuki ndio unaofanya dhabihu nyingi zisikubalike. Yawezekana Kaini alikwenda mbele za Bwana na moyo kama huu. Bwana hakupokea dhabihu yake. Sisi tutambue kwamba ni wajibu wetu kutoa dhabihu mbele ya Bwana. Sisi tuje mbele ya Bwana, tuondoe chuki, na hasira na uchoyo. Uchoyo unaotukumba wengi ni kukataa kutoa muda Wetu kwa Bwana. Kuna wakati kweli tunanogewa na kazi, kazi inanoga tunamtupa Bwana pembeni. Pia tunakuja na chuki sana na wengine-mbele ya Yesu hakuna haja ya kuhifadhi chuki kabisa. Huu ndio udhaifu wetu, lakini inatupasa kuuleza mbele ya Bwana, tuukubali udhaifu huu. Tumuombe atusaidie. Kwenye somo la Injili, Yesu anakataa kuwapatia ishara Wafarisayo. Yesu anakataa kuwapa ishara kwani hii ilikuwa ni ishara kwa wasio na Imani, walitaka kumjaribu. Kati ya vitu anavyovichukia Yesu ni kutaka kujaribiwa. Yeye anatenda muujiza kwa aliye na imani. Hata siku moja hatendi muujiza kwa asiye na imani. Hiki kilichowapata mafarisayo ndicho kinachotutokea na sisi kila siku ndugu zangu. Wengi wetu hatujibiwi kwa sababu tunakwenda mbele ya Yesu bila imani. Ukosefu wa unyofu unatukosesha mengi, tukiwa mbele ya Yesu ni lazima tuoneshe unyofu. Yesu alisema heri walio wanyofu wa moyo, maana watamuona Mungu. Unyofu wa moyo ni kuishi kiapo chako bila kuonesha ufarisayo, bila kuwa ndumila kuwili, kama ni watu wa ndoa tunaishi kama watu wa ndoa kweli. Sisi tukazane kuwa wanyofu. Unyofu ni ufunguo wa baraka maishani mwetu. ©️Pd. Prosper Kessy OFMCap.

Post image
Image
Tanzanian Catholics Online
Tanzanian Catholics Online
2/22/2025, 7:24:25 PM
Post image
Image
Link copied to clipboard!