UwepoTv
UwepoTv
February 15, 2025 at 06:10 AM
*SOMA NENO, HUBIRI NENO, OMBA BILA AIBU* Bwana Yesu Kristo asifiwe, Kuna Mtu anaona aibu kuomba mbele za watu, anaona aibu kushuhudia matendo makuu ya Mungu, ZAIDI ANAONA AIBU KUSEMA AMEOKOKA AMEMPOKEA YESU KRISTO Kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yake. *Sasa soma* 1. _Warumi 1:16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia._ *Yesu Kristo anasema tena* 2. _Mathayo 10:33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni._ Shabbat shalom KADOSH KADOSH KADOSH ADONAIY T'VAOTH Barikiwa SERVANT: Franklin_Henocko EBENEZER Shalom Ministry
Image from UwepoTv: *SOMA NENO, HUBIRI NENO, OMBA BILA AIBU*  Bwana Yesu Kristo asifiwe, K...
👍 🙏 2

Comments