
SOKALOJIA
January 31, 2025 at 04:04 AM
✍🏻 Sheria Namba Moja Ya Mpira Wa Miguu inazungumzia Eneo la Kuchezea, Yaani Uwanja. Hebu tujikumbushe kidogo kuhusiana na Sehemu kuu za Uwanja, Ulalo na Wima.
✍🏻 Kwa Ulalo (Horizontal), Uwanja wa mpira wa miguu unagawanyika katika sehemu tatu, ambazo ni:
1. Nusu Ya Kwanza (Defensive Third) – Golikipa na Walinzi hii ndo Sehemu yao ya kujidai.
2. Nusu Ya Pili (Middle Third) – Viungo Walinzi, Viungo Washambuliaji na Viungo Wa Pembeni, hapa ndio Sehemu huonyesha Ufundi wao.
3. Nusu Ya Tatu (Attacking Third) –
Washambuliaji hutumia eneo hili kufumania Nyavu.
✍🏻 Kwa Wima (Vertical), Uwanja wa Mpira Wa Miguu Unagawanyika Katika Sehemu tano🤯, ambazo ni:
1. Winga Ya Kulia ( Right Wing/Flank)
2. Winga Ya Kushoto ( Left Wing/Flank)
3. Nusu Nafasi Ya Kulia ( Right Halfspace)
4. Nusu Nafasi Ya Kushoto (Left Halfspace)
5. Katikati (Centre).
✍🏻 Unakitu cha kufundisha kuhusiana na Soka?, Wasiliana Nami kupitia Simu No. 0760728723 (WhatsApp).
#lielewesoka.
❤️
🔥
3