
SOKALOJIA
16 subscribers
About SOKALOJIA
βͺοΈDarasa Huru Kuhusiana na SOKA,, Kwenye hili Darasa,Kila Mtu ni Mwalimu. βͺοΈ Lugha Rafiki ni Kipaumbele Chetu. #lielewesoka.
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

REST DEFENCE & REST ATTACK. βπ» Rest Defence (Muundo Wa ulinzi wakati timu inashambulia). βπ» Ni jinsi timu inavyojiweka kimkakati 'wakati ipo na mpira' ili kuzuia mashambulizi ya kushtukiza (counterattacks) ikiwa itapoteza umiliki wa mpira. βπ» Rest Defence, inaundwa na wachezaji wote waliopo nyuma ya msitari wa washambuliaji, e.g, Timu ambayo ikiwa kwenye nusu ya Mwisho inakuwa na Muundo wa 3-2-5, wanaounda Rest Defence ni hawa 3-2. ( Picha hapo juu βπ» ) DHUMUNI NI.. inaendelea.....


Huwa unazijua maana ya hivi vifupisho?ππ»ππ»


Endelea...... Christensen, Araujo, na Kounde, Kwenye Back 3. De Jong, anatoka kiungo wa kulia, anashuka chini Kuungana na Busquets, kutengeneza namba 6 wawili. Gavi, anatoka Winga wa kushoto, anaingia ndani kuungana na Pedri, kutengeneza namba 8 wawili. Balde, anatoka kuwa beki wa kushoto, anasogea juu kuungana na Lewandowski na Dembele. βπ» Picha no.1, Kocha amepanga wachezaji ili waenee kwenye kikosi (Huo ni Mfumo). Picha no. 2, Wachezaji wakiwa katika muundo wa uchezaji kulingana na majukumu yao, kwa kuzingatia ubora wao katika maeneo waliyopo ( Huo ndio Muundo) βπ» Kumbuka: Mfumo unaweza ukawa ni 4-4-2. na muundo wa uchezaji ukawa 4-4-2 pia, Namaanisha 'muundo wa uchezaji siyo lazima ubadilike.' MUUNDO UNATOKEA WAPI?. βπ» Kocha anapoingia kwenye timu mpya, ili atengeneze muundo wa uchezaji lazima azingatie... A. Falsafa: picha ya namna timu yake anataka icheze.. - Kumiliki mpira ( Possession based ball) - Kuzuia na kushambulia kwa Kushtukiza - Totall Football, n.k B. Muktadha/Mazingira ( Context ): lazima ajiulize maswali kama:- βπ» kundi la wachezaji nilio nao wanasifa gani?.. βπ»Wanaweza kucheza aina ya mpira ninaoutaka?....kama.. A. NDIYO: hatua ya kwanza.. βπ» anza kufundisha aina ya soka unalolitaka kwa kuzingatia nafasi za wachezaji, ( Kama ni beki wa kushoto muache acheze kama beki wa kushoto, au ni winga anayetumia mguu wa kulia na anapenda kutokea kulia muache acheze kama winga wa kulia), anza na nafasi zao walizozoea, lakini anza kuingiza aina ya mpira unaotaka kwenye akili zao. βπ» Lengo ni uelewe Uimara na udhaifu wa kila Mchezaji, ukishaelewa ubora na udhaifu wa kila mchezaji hatua ya pili... βπ» Tambua ni wachezaji wapi hawawezi kuendana na aina ya mpira unaoutaka, na anza kuwaondoa kwenye kikosi bila kujali ubora wao kwa muda huo ( siyo kila mchezaji mzuri/bora, anaweza kucheza katika kila muundo wa uchezaji). hatua ya tatu.... βπ» Tengeneza Muundo Wa Uchezaji, Kwa kuzingatia Majukumu yanayong'arisha ubora wa mchezaji na kuficha udhaifu wake, kwa Mchezaji Mmoja mmoja hadi timu nzima. βπ» Zingatia: Uwezo wa Mchezaji "A", Uimalishe Uwezo wa Mchezaji "B." Hatua ya Nne.... βπ» Baada Muundo Wa Uchezaji kuimarika/kuiva, ndio wakati kocha anatakiwa aendelee kuboresha muundo kwa kuuliza maswali tofautitofauti kulingana na uimara na udhaifu wa Kila mpinzani. KIVIPI UNABORESHA MUUNDO. 1. USAJILI. βπ» Ondoa wachezaji ambao, uwezo wao umepungua kutokana na Umri au Mahitaji, (Sir Alex Ferguson alikuwa bora Sana katika eneo hili) βπ» Boresha Maeneo imara kwa kuongeza Ubora Sawa au Zaidi ya uliopo, ( ushindani ) 2. UBUNIFU. βπ» Kila mara ibuka na mbinu mpya (epuka kuzoeleka). ITAENDELEA..... #LIELEWESOKA.

NJE NDANI, MUUNDO WA UCHEZAJI. βπ» Mara nyingi Wachambuzi wa Soka, Utawasikia Wanasema, "Muundo Wa timu "X," Haueleweki, au timu "Y," ina Muundo Mzuri Wa Uchezaji. Muundo Wa Uchezaji ni nini?, tunaujuaje huu ni muundo wa timu fulani?, Je, kuna tofauti kati ya 'Muundo Wa Uchezaji' na 'Mfumo'?. βπ» ili tuelewe Vizuri Muundo Wa Uchezaji, tuanze kukumbushana Kwanza, Maana ya Mfumo... βπ» Mfumo: Ni mpangilio wa kiufundi wa timu uwanjani, ukionyesha idadi ya wachezaji katika eneo la.... Ulinzi, Kiungo, na Ushambuliaji. Mfano: Barcelona katika Mfumo wa 4-3-3 (picha hapoππ» juu..) Back 4 ni..Balde(LB), Christensen(LCB), Araujo(RCB), Kounde(RB). Viungo ni...Busquets(DM), De Jong(LCM), Pedri(RCM). Washambuliaji... Gavi(LW), Lewandowski(C.F), Dembele(RW) LAKINI... βπ» Muundo wa Uchezaji: Ni namna timu inavyopanga wachezaji wake uwanjani kwa mujibu wa majukumu yao, wakiwa na mpira (in Possession). Mfano: Barcelona Katika Muundo wa Uchezaji 3-2-2-3 (picha katika post hapo ππ»ππ» chini..)


VIFUPISHO VYA NAFASI ZA WACHEZAJI UWANJANI. βπ» Najua unajua, lakini Wacha tukumbushane kidogo GK - (Goalkeeper) β Kipa CB - (Center Back) β Beki wa Kati LB - (Left Back) β Beki wa Kushoto RB - (Right Back) β Beki wa Kulia LWB - (Left Wing Back) β Beki wa Mrengo wa Kushoto RWB - (Right Wing Back) β Beki wa Mrengo wa Kulia CDM - (Central Defensive Midfielder) β Kiungo Mkabaji wa Kati CM - (Central Midfielder) β Kiungo wa Kati CAM - (Central Attacking Midfielder) β Kiungo Mshambuliaji wa Kati LM - (Left Midfielder) β Kiungo wa Kushoto RM - (Right Midfielder) β Kiungo wa Kulia LW - (Left Winger) β Winga wa Kushoto RW - (Right Winger) β Winga wa Kulia CF - (Center Forward) β Mshambuliaji wa Kati ST - (Striker) β Mshambuliaji ------------------------------------------------ FB - (Full Back) β Beki wa Pembeni (Beki wa Kushoto au Beki wa Kulia) WB - (Wing Back) β Beki wa Mrengo (Beki wa Mrengo wa Kushoto au Beki wa Mrengo wa Kulia) DM - (Defensive Midfielder) β Kiungo Mkabaji AM - (Attacking Midfielder) β Kiungo Mshambuliaji SS - (Second Striker) β Mshambuliaji wa Pili AF - (Advanced Forward) β Mshambuliaji wa Juu TM - (Target Man) β Mshambuliaji wa Kirefu IF - (Inverted Forward) β Mshambuliaji wa Ndani IWB - (Inverted Wing Back) β Beki wa Mrengo wa Ndani CD - (Center-Back) β Beki wa Kati (mbadala wa CB) RDM/LDM - (Right Defensive Midfielder/Left Defensive Midfielder) β Kiungo Mkabaji wa Kulia/Kiungo Mkabaji wa Kushoto RCB/LCB - (Right Center-Back/Left Center-Back) β Beki wa Kati wa Kulia/Beki wa Kati wa Kushoto. #LIELEWESOKA.

MISINGI/FALSAFA NA MIFUMO (PRINCIPALS & FORMATIONS) βπ» Msimu Wa 2023/2024 (Kwa ligi kuu ya Uingereza,EPL.), Vincent Kompany(Alikuwa Kocha Wa Burnley), Alikumbana na Chanagamoto ya Kuishusha daraja Burnley, Baada ya kumaliza katika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi. βπ» Siku Chache baadae ilitokea taarifa ya kushangaza kwa Wapenda Soka wengi, Baada ya Vincent Kompany, kutangazwa Kuwa Kocha Mkuu Kwa Vigogo vya Kandanda Nchini Ujerumani, Beryen Munich. βπ» Moja kati ya Swali lililochosha Ubongo wa Wengi ni, "inakuwaje Kocha aliyeishusha Daraja Burnley, anapewa nafasi ya kuwa Kocha Mkuu katika Moja ya Klabu Kubwa Duniani, Beryen Munich?. Tena ndani ya siku chache Sana!. βπ» Naamini, Moja kati Ya Sababu iliyompa hatamu Vincent Kompany Kwa Vigogo hivyo vya Ujerumani ni "Misingi/Falsafa Yake Katika Soka ." βπ» "Misingi/Falsafa π€―", Yes!. Naomba dakika zako chache tu, nikwambie kuhusiana na hivi vitu viwili, "MISINGI/FALSAFA" NA "MIFUMO" Kwenye Soka. βπ» Misingi/ Falsafa: Huu ni mtazamo wa kocha kuhusu namna timu yake inapaswa kucheza. Inahusisha imani yake juu ya soka, kama vile:- A. Possession Football β Pep Guardiola Kuhifadhi mpira kwa muda mrefu, pasi fupi na haraka, na kushambulia kwa uvumilivu. Mfano: Barcelona (2008β2012), Bayern Munich, Manchester City. B. Total Football β Johan Cruyff & Rinus Michels Wachezaji wanabadilishana nafasi uwanjani kulingana na mahitaji ya mchezo, mtindo wa kushambulia kwa uhuru. Mfano: Ajax, Barcelona (1980s-1990s). C. Park the Bus β JosΓ© Mourinho Kujilinda kwa wachezaji wengi, kucheza kwa nidhamu, na kushambulia kwa kushtukiza. ________________________________ βπ» Mfumo: Huu ni mpangilio wa kiufundi wa timu uwanjani, ukionyesha idadi ya wachezaji katika kila eneo. Mfumo maarufu ni kama 4-3-3, 4-4-2, au 3-5-2. Mfumo huu huathiri jinsi timu inavyoshambulia na kujilinda. βπ» Kocha anaweza akawa anaamini katika, Falsafa ya Kujilinda Sana na Akatumia Mfumo wa 4-3-3. inaaminika 4-4-2 Ni Mfumo ambao ni Mzuri Sana Kuzuia, lakini Pep Guardiola, aliwahi kutumia 4-4-2, na bado akabaki kwenye msingi Wake wa Kumiliki Mpira. CHUKUA HII: βπ» Mfumo unaweza kubadilika kutokana na Sifa Za Wachezaji, Lakini Misingi/Falsafa Ya Kocha huwa haibadiliki, Mfano JosΓ© Mourinho, Mpatie Mancity, Arsenal au Barcelona na Aina ya wachezaji waliopo kwenye Vilabu hivyo kwasasa, anaweza kubadilisha Mifumo, lakini bado atafundisha Falsafa yake ambayo ni " kujilinda na idadi kubwa ya Wachezaji na kushambulia kwa Kushtukiza." π Misingi/Falsafa ya kocha, ndio inayoamua Timu icheze aina gani ya Mpira. Mifumo ni kama ramani tu ya Utekelezaji wa Misingi ya Kocha. βπ» Misingi/Falsafa ya kocha "X" Inaweza ikaendana na Misingi/Falsafa ya Klabu "A", na hivyo ikawa rahisi kwa Kocha "X" kufanya kazi pamoja na Klabu "A." #LIELEWESOKA.

DHUMUNI NI.. A. kuhakikisha ulinzi unadumu hata wakati wa kushambulia kwa... 1. kufunga mianya ya pasi. 2. kujilinda dhidi ya mpito ( transition ), kwa kuingilia mipira (interception), na kuchelewesha mashambulizi ya wapinzani, kupitia faulo za kiufundi, na kubana eneo Bora la mpinzani ( ndani? au pembeni? ) anapofanya mashambulizi ya kushtukiza. B. Kudumisha umiliki wa mpira na mashambulizi, kwa kuwa karibukaribu ili... 1. kupora mipira haraka pale inapopotea (Counter pressing). 2. kuwe na mfululizo wa pasi fupi fupi ambazo siyo rahisi kuwa-intercepted. REST ATTACK βπ» Rest attack ni muundo wa kushambulia ambao timu inauweka wakati wa kujilinda ( Hawana mpira ). lengo ni kuhakikisha wanakuwa tayari kushambulia mara tu wanapopata mpira tena. (Picha hapo chini ππ»ππ») Misingi ya Rest Attack: 1. Upangaji wa Wachezaji kwa Mkakati β Wakati timu inajilinda, baadhi ya wachezaji wanabaki katika nafasi za mbele au pembeni ili kuhakikisha kuwa timu inaweza kushambulia haraka pindi mpira unapopatikana, ( mshambuliaji mmoja au wawili.) 2. Mpito wa Haraka (Transition Play) β timu inapaswa kubadilika haraka kutoka kujilinda kwenda kushambulia. Wachezaji waelewe majukumu yao na kufanya maamuzi ya haraka pindi timu inaponyakua mpira. 3. Kuvunja Mfumo wa Mpinzani β Kwa kutathmini jinsi mpinzani anavyojipanga kujilinda, na kulenga maeneo dhaifu na kutumia kasi ya mpito kushambulia kwa mafanikio. βπ» ili Rest Attack ifanikiwe, Mshambuliaji/Target Player, awe na uwezo wa kucheza lango la timu Pinzani akiwa amelitega mgongo. βͺοΈErling Haaland (Man City) βͺοΈ Alexander Isak ( Newcastle United ) βͺοΈJamie Vardy (Leicester City) βͺοΈFilippo Inzaghi (AC Milan, Juventus) #LIELEWESOKA.

βπ» Sheria Namba Moja Ya Mpira Wa Miguu inazungumzia Eneo la Kuchezea, Yaani Uwanja. Hebu tujikumbushe kidogo kuhusiana na Sehemu kuu za Uwanja, Ulalo na Wima. βπ» Kwa Ulalo (Horizontal), Uwanja wa mpira wa miguu unagawanyika katika sehemu tatu, ambazo ni: 1. Nusu Ya Kwanza (Defensive Third) β Golikipa na Walinzi hii ndo Sehemu yao ya kujidai. 2. Nusu Ya Pili (Middle Third) β Viungo Walinzi, Viungo Washambuliaji na Viungo Wa Pembeni, hapa ndio Sehemu huonyesha Ufundi wao. 3. Nusu Ya Tatu (Attacking Third) β Washambuliaji hutumia eneo hili kufumania Nyavu. βπ» Kwa Wima (Vertical), Uwanja wa Mpira Wa Miguu Unagawanyika Katika Sehemu tanoπ€―, ambazo ni: 1. Winga Ya Kulia ( Right Wing/Flank) 2. Winga Ya Kushoto ( Left Wing/Flank) 3. Nusu Nafasi Ya Kulia ( Right Halfspace) 4. Nusu Nafasi Ya Kushoto (Left Halfspace) 5. Katikati (Centre). βπ» Unakitu cha kufundisha kuhusiana na Soka?, Wasiliana Nami kupitia Simu No. 0760728723 (WhatsApp). #LIELEWESOKA.