SOKALOJIA
SOKALOJIA
February 2, 2025 at 10:16 PM
MISINGI/FALSAFA NA MIFUMO (PRINCIPALS & FORMATIONS) ✍🏻 Msimu Wa 2023/2024 (Kwa ligi kuu ya Uingereza,EPL.), Vincent Kompany(Alikuwa Kocha Wa Burnley), Alikumbana na Chanagamoto ya Kuishusha daraja Burnley, Baada ya kumaliza katika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi. ✍🏻 Siku Chache baadae ilitokea taarifa ya kushangaza kwa Wapenda Soka wengi, Baada ya Vincent Kompany, kutangazwa Kuwa Kocha Mkuu Kwa Vigogo vya Kandanda Nchini Ujerumani, Beryen Munich. ✍🏻 Moja kati ya Swali lililochosha Ubongo wa Wengi ni, "inakuwaje Kocha aliyeishusha Daraja Burnley, anapewa nafasi ya kuwa Kocha Mkuu katika Moja ya Klabu Kubwa Duniani, Beryen Munich?. Tena ndani ya siku chache Sana!. ✍🏻 Naamini, Moja kati Ya Sababu iliyompa hatamu Vincent Kompany Kwa Vigogo hivyo vya Ujerumani ni "Misingi/Falsafa Yake Katika Soka ." ✍🏻 "Misingi/Falsafa 🤯", Yes!. Naomba dakika zako chache tu, nikwambie kuhusiana na hivi vitu viwili, "MISINGI/FALSAFA" NA "MIFUMO" Kwenye Soka. ✍🏻 Misingi/ Falsafa: Huu ni mtazamo wa kocha kuhusu namna timu yake inapaswa kucheza. Inahusisha imani yake juu ya soka, kama vile:- A. Possession Football – Pep Guardiola Kuhifadhi mpira kwa muda mrefu, pasi fupi na haraka, na kushambulia kwa uvumilivu. Mfano: Barcelona (2008–2012), Bayern Munich, Manchester City. B. Total Football – Johan Cruyff & Rinus Michels Wachezaji wanabadilishana nafasi uwanjani kulingana na mahitaji ya mchezo, mtindo wa kushambulia kwa uhuru. Mfano: Ajax, Barcelona (1980s-1990s). C. Park the Bus – José Mourinho Kujilinda kwa wachezaji wengi, kucheza kwa nidhamu, na kushambulia kwa kushtukiza. ________________________________ ✍🏻 Mfumo: Huu ni mpangilio wa kiufundi wa timu uwanjani, ukionyesha idadi ya wachezaji katika kila eneo. Mfumo maarufu ni kama 4-3-3, 4-4-2, au 3-5-2. Mfumo huu huathiri jinsi timu inavyoshambulia na kujilinda. ✍🏻 Kocha anaweza akawa anaamini katika, Falsafa ya Kujilinda Sana na Akatumia Mfumo wa 4-3-3. inaaminika 4-4-2 Ni Mfumo ambao ni Mzuri Sana Kuzuia, lakini Pep Guardiola, aliwahi kutumia 4-4-2, na bado akabaki kwenye msingi Wake wa Kumiliki Mpira. CHUKUA HII: ✍🏻 Mfumo unaweza kubadilika kutokana na Sifa Za Wachezaji, Lakini Misingi/Falsafa Ya Kocha huwa haibadiliki, Mfano José Mourinho, Mpatie Mancity, Arsenal au Barcelona na Aina ya wachezaji waliopo kwenye Vilabu hivyo kwasasa, anaweza kubadilisha Mifumo, lakini bado atafundisha Falsafa yake ambayo ni " kujilinda na idadi kubwa ya Wachezaji na kushambulia kwa Kushtukiza." 📍 Misingi/Falsafa ya kocha, ndio inayoamua Timu icheze aina gani ya Mpira. Mifumo ni kama ramani tu ya Utekelezaji wa Misingi ya Kocha. ✍🏻 Misingi/Falsafa ya kocha "X" Inaweza ikaendana na Misingi/Falsafa ya Klabu "A", na hivyo ikawa rahisi kwa Kocha "X" kufanya kazi pamoja na Klabu "A." #lielewesoka.
🔥 ❤️ 👏 4

Comments