
SOKALOJIA
February 4, 2025 at 07:09 PM
NJE NDANI, MUUNDO WA UCHEZAJI.
✍🏻 Mara nyingi Wachambuzi wa Soka, Utawasikia Wanasema, "Muundo Wa timu "X," Haueleweki, au timu "Y," ina Muundo Mzuri Wa Uchezaji. Muundo Wa Uchezaji ni nini?, tunaujuaje huu ni muundo wa timu fulani?, Je, kuna tofauti kati ya 'Muundo Wa Uchezaji' na 'Mfumo'?.
✍🏻 ili tuelewe Vizuri Muundo Wa Uchezaji, tuanze kukumbushana Kwanza, Maana ya Mfumo...
✍🏻 Mfumo: Ni mpangilio wa kiufundi wa timu uwanjani, ukionyesha idadi ya wachezaji katika eneo la.... Ulinzi, Kiungo, na Ushambuliaji.
Mfano: Barcelona katika Mfumo wa 4-3-3 (picha hapo👆🏻 juu..)
Back 4 ni..Balde(LB), Christensen(LCB), Araujo(RCB), Kounde(RB).
Viungo ni...Busquets(DM), De Jong(LCM), Pedri(RCM).
Washambuliaji... Gavi(LW), Lewandowski(C.F), Dembele(RW)
LAKINI...
✍🏻 Muundo wa Uchezaji: Ni namna timu inavyopanga wachezaji wake uwanjani kwa mujibu wa majukumu yao, wakiwa na mpira (in Possession).
Mfano: Barcelona Katika Muundo wa Uchezaji 3-2-2-3 (picha katika post hapo 👇🏻👇🏻 chini..)

❤️
🔥
2