SOKALOJIA
SOKALOJIA
February 4, 2025 at 07:12 PM
Endelea...... Christensen, Araujo, na Kounde, Kwenye Back 3. De Jong, anatoka kiungo wa kulia, anashuka chini Kuungana na Busquets, kutengeneza namba 6 wawili. Gavi, anatoka Winga wa kushoto, anaingia ndani kuungana na Pedri, kutengeneza namba 8 wawili. Balde, anatoka kuwa beki wa kushoto, anasogea juu kuungana na Lewandowski na Dembele. ✍🏻 Picha no.1, Kocha amepanga wachezaji ili waenee kwenye kikosi (Huo ni Mfumo). Picha no. 2, Wachezaji wakiwa katika muundo wa uchezaji kulingana na majukumu yao, kwa kuzingatia ubora wao katika maeneo waliyopo ( Huo ndio Muundo) ✍🏻 Kumbuka: Mfumo unaweza ukawa ni 4-4-2. na muundo wa uchezaji ukawa 4-4-2 pia, Namaanisha 'muundo wa uchezaji siyo lazima ubadilike.' MUUNDO UNATOKEA WAPI?. ✍🏻 Kocha anapoingia kwenye timu mpya, ili atengeneze muundo wa uchezaji lazima azingatie... A. Falsafa: picha ya namna timu yake anataka icheze.. - Kumiliki mpira ( Possession based ball) - Kuzuia na kushambulia kwa Kushtukiza - Totall Football, n.k B. Muktadha/Mazingira ( Context ): lazima ajiulize maswali kama:- ✍🏻 kundi la wachezaji nilio nao wanasifa gani?.. ✍🏻Wanaweza kucheza aina ya mpira ninaoutaka?....kama.. A. NDIYO: hatua ya kwanza.. ✍🏻 anza kufundisha aina ya soka unalolitaka kwa kuzingatia nafasi za wachezaji, ( Kama ni beki wa kushoto muache acheze kama beki wa kushoto, au ni winga anayetumia mguu wa kulia na anapenda kutokea kulia muache acheze kama winga wa kulia), anza na nafasi zao walizozoea, lakini anza kuingiza aina ya mpira unaotaka kwenye akili zao. ✍🏻 Lengo ni uelewe Uimara na udhaifu wa kila Mchezaji, ukishaelewa ubora na udhaifu wa kila mchezaji hatua ya pili... ✍🏻 Tambua ni wachezaji wapi hawawezi kuendana na aina ya mpira unaoutaka, na anza kuwaondoa kwenye kikosi bila kujali ubora wao kwa muda huo ( siyo kila mchezaji mzuri/bora, anaweza kucheza katika kila muundo wa uchezaji). hatua ya tatu.... ✍🏻 Tengeneza Muundo Wa Uchezaji, Kwa kuzingatia Majukumu yanayong'arisha ubora wa mchezaji na kuficha udhaifu wake, kwa Mchezaji Mmoja mmoja hadi timu nzima. ✍🏻 Zingatia: Uwezo wa Mchezaji "A", Uimalishe Uwezo wa Mchezaji "B." Hatua ya Nne.... ✍🏻 Baada Muundo Wa Uchezaji kuimarika/kuiva, ndio wakati kocha anatakiwa aendelee kuboresha muundo kwa kuuliza maswali tofautitofauti kulingana na uimara na udhaifu wa Kila mpinzani. KIVIPI UNABORESHA MUUNDO. 1. USAJILI. ✍🏻 Ondoa wachezaji ambao, uwezo wao umepungua kutokana na Umri au Mahitaji, (Sir Alex Ferguson alikuwa bora Sana katika eneo hili) ✍🏻 Boresha Maeneo imara kwa kuongeza Ubora Sawa au Zaidi ya uliopo, ( ushindani ) 2. UBUNIFU. ✍🏻 Kila mara ibuka na mbinu mpya (epuka kuzoeleka). ITAENDELEA..... #lielewesoka.
❤️ 👍 🔥 🤯 4

Comments