SOKALOJIA
SOKALOJIA
February 11, 2025 at 01:07 AM
DHUMUNI NI.. A. kuhakikisha ulinzi unadumu hata wakati wa kushambulia kwa... 1. kufunga mianya ya pasi. 2. kujilinda dhidi ya mpito ( transition ), kwa kuingilia mipira (interception), na kuchelewesha mashambulizi ya wapinzani, kupitia faulo za kiufundi, na kubana eneo Bora la mpinzani ( ndani? au pembeni? ) anapofanya mashambulizi ya kushtukiza. B. Kudumisha umiliki wa mpira na mashambulizi, kwa kuwa karibukaribu ili... 1. kupora mipira haraka pale inapopotea (Counter pressing). 2. kuwe na mfululizo wa pasi fupi fupi ambazo siyo rahisi kuwa-intercepted. REST ATTACK ✍🏻 Rest attack ni muundo wa kushambulia ambao timu inauweka wakati wa kujilinda ( Hawana mpira ). lengo ni kuhakikisha wanakuwa tayari kushambulia mara tu wanapopata mpira tena. (Picha hapo chini 👇🏻👇🏻) Misingi ya Rest Attack: 1. Upangaji wa Wachezaji kwa Mkakati – Wakati timu inajilinda, baadhi ya wachezaji wanabaki katika nafasi za mbele au pembeni ili kuhakikisha kuwa timu inaweza kushambulia haraka pindi mpira unapopatikana, ( mshambuliaji mmoja au wawili.) 2. Mpito wa Haraka (Transition Play) – timu inapaswa kubadilika haraka kutoka kujilinda kwenda kushambulia. Wachezaji waelewe majukumu yao na kufanya maamuzi ya haraka pindi timu inaponyakua mpira. 3. Kuvunja Mfumo wa Mpinzani – Kwa kutathmini jinsi mpinzani anavyojipanga kujilinda, na kulenga maeneo dhaifu na kutumia kasi ya mpito kushambulia kwa mafanikio. ✍🏻 ili Rest Attack ifanikiwe, Mshambuliaji/Target Player, awe na uwezo wa kucheza lango la timu Pinzani akiwa amelitega mgongo. ▪️Erling Haaland (Man City) ▪️ Alexander Isak ( Newcastle United ) ▪️Jamie Vardy (Leicester City) ▪️Filippo Inzaghi (AC Milan, Juventus) #lielewesoka.
❤️ 🔥 2

Comments