
START TEK
February 24, 2025 at 01:21 PM
Kwa Nini Watu Walianza Kutumia Noti za Karatasi?
Katika karne ya 7, wakati wa Nasaba ya Tang, wafanyabiashara wakubwa walianza kutumia risiti za karatasi kufanya malipo kati yao, badala ya kubeba sarafu za chuma. Sarafu hizo ziliwekwa kwa usalama kwa watu waliowaamini.
Ifikapo karne ya 10, wakati wa Nasaba ya Song, kulikuwa na upungufu wa shaba kwa ajili ya kutengeneza sarafu. Kutokana na hali hiyo, baadhi ya taasisi zilizokuwa zinatunza sarafu zilipatiwa haki ya kutoa noti za benki kama mbadala wa sarafu za chuma.
Ilikuwa hadi mwaka 1120 ambapo serikali kuu ilianza rasmi kuchapisha na kusambaza noti zake za karatasi, hatua iliyoashiria mwanzo wa sarafu za karatasi tunazotumia leo.
🔹 Endelea kufuatilia PrimePursuits kwa maarifa, fursa na taarifa muhimu!
📢 SHARE na wengine ili nao wajifunze!
