GSM Group
GSM Group
February 9, 2025 at 09:20 AM
Katika kuendeleza jitihada za kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini Tanzania, Taasisi ya GSM Foundation imeshiriki katika mahafali ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Bagamoyo yaliyofanyika tarehe 6 Februari 2025. Akizungumza katika hafla hiyo akiwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa GSM Foundation, Bi. Faith Gugu ameupongeza uongozi wa shule hiyo chini ya Mwl. Mkuu Bw. Method Kunambi, kwa kazi nzuri wanayoifanya kuinua ufaulu na malezi mazuri ya wanafunzi wa shule hiyo. Aidha, alipokea maombi ya changamoto mbalimbali za shule hiyo, na kuahidi kuwa Taasisi ya GSM Foundation itachangia 1. Shilingi milioni kumi za Kitanzania kwa ajili ya vifaa vya TEHAMA 2. Vifaa vya michezo 3. ⁠pamoja na vitabu vinavyohitajika shuleni Taasisi ya GSM Foundation pia imeahidi kuendelea kushirikiana na shule hiyo katika kutatua changamoto nyingine zinazoikabili shule hio. Gsm Foundation,builds you to build others.

Comments