๐ ๐ฟ ๐๐ต๐ฎ๐ธ๐๐๐ต๐ฎ๐ป๐ด๐ฎ๐๐ฎ ๐๐น๐ถ๐บ๐ ๐ฆ๐ผ๐น๐๐๐ถ๐ผ๐ป๐
February 16, 2025 at 04:21 AM
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI โ JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatangaza nafasi za ajira kwa vijana wenye sifa stahiki. Nafasi hizi ni kwa wale wenye elimu ya kidato cha nne, sita na shahada, na pia kwa wale wenye ujuzi katika fani mbalimbali.
1. Wenye Elimu ya Kidato cha Nne
Sifa za mwombaji:
โ
Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
โ
Awe na cheti cha kuzaliwa
โ
Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
โ
Awe na afya njema kimwili na kiakili
โ
Asiwe na kumbukumbu za uhalifu
โ
Awe hajaoa/kuolewa
โ
Asiwe na alama za kuchora mwilini (tattoo)
โ
Asiwe ametumia madawa ya kulevya
โ
Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya Zimamoto na Uokoaji
โ
Awe hajawahi kuajiriwa serikalini
โ
Urefu wa kiume: futi 5.7 na wa kike: futi 5.4
โ
Awe tayari kugharamia hatua zote za usaili
โ
Umri: miaka 18 โ 25
2. Wenye Elimu ya Kidato cha Nne/Sita na Ujuzi Maalum
Fani zinazohitajika ni:
โ๏ธ Udereva wa magari makubwa (leseni daraja E, umri 18-28)
โ๏ธ Ufundi bomba
โ๏ธ Uuguzi
โ๏ธ Taaluma ya Zimamoto na Uokoaji
โ๏ธ Utabibu
โ๏ธ Urubani wa Helikopta (umri 18-35)
3. Wenye Shahada
Fani zinazohitajika ni:
โ๏ธ Uhandisi Bahari (Marine Engineering)
โ๏ธ TEHAMA
โ๏ธ Uhandisi wa Ndege (Aircraft Maintenance)
โ๏ธ Lugha (Kiingereza)
โ๏ธ Ukadiriaji Majenzi (QS)
โ๏ธ Teknolojia ya Habari (Multi-Media Technology)
โ๏ธ Uchumi
โ๏ธ Sheria
โ๏ธ Ualimu (Education Management)
โ๏ธ Usafirishaji (Road & Railway Transport Logistics)
โ๏ธ Uhandisi wa Kemikali (Chemical Processing)
Sifa:
โ๏ธ Sifa zote za waombaji wa kidato cha nne
โ๏ธ Umri: miaka 18 โ 28
4. Namna ya Kufanya Maombi
โ
Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaopatikana kupitia kiunga ajira.zimamoto.go.tz
โ
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 28 Februari 2025
โ
Mwombaji anapaswa kuambatisha:
๐ Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono
๐ Nakala ya cheti cha kuzaliwa
๐ Fomu ya uthibitisho wa afya kutoka kwa daktari wa serikali
๐ Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA
๐ Picha ya pasipoti ya hivi karibuni
๐ Namba ya mtihani wa kidato cha nne/sita
๐ Nakala ya vyeti vya elimu (kwa waombaji wa shahada)
๐ Barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa
Maelezo Muhimu
โ Nakala za vyeti lazima zithibitishwe na Kamishna wa Viapo au Hakimu
โ Maombi yanayowasilishwa kwa njia ya posta, mkono au barua pepe hayatapokelewa
โ Mwombaji atakayewasilisha nyaraka za kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria
๐ด Unahitaji msaada wa kutuma maombi? Wasiliana na Mr. Chakushangaza kwa namba 0627368679 kwa msaada wa kufungua akaunti na kutuma maombi yako kwa usahihi.