
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
February 7, 2025 at 10:03 AM
Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) limekutana na kufanya kikao kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yatakayosaidia kuboresha huduma na utendaji kazi wa Taasisi hiyo.
Kikao hicho kimefanyika Februari 06, 2025 chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Herbert Makoye ambaye ni Mkuu wa Taasisi hiyo.
Dkt. Makoye amewataka watumishi kuendelea kuchapa kazi kwa weledi na kwa ushirikiano ili kuendana na dhana ya 'TaSUBa Kituo chenye Ubora Uliotukuka Afrika Mashariki.'
