
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
February 28, 2025 at 10:00 PM
Wanafunzi katoka Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) cha Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam wametembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Februari 28, 2025 ikiwa ni ziara ya kimasomo ili kutimiza matakwa ya makubaliano (MoU) kati ya vyuo hivyo viwili.
Makubaliano ambayo TaSUBa iliingia na TCTA yanahusisha utoaji wa mafunzo kwa kipindi cha muda mfupi kisichopungua mwezi mmoja na kisichozidi miezi sita kwa kila udhahili.
Makubaliano hayo yanahitaji wanafunzi kutoka TCTA kutembelea TaSUBa ili kujifunza mazingira ya Taasisi hiyo kabla ya kuhitimu mafunzo angalau mara moja kwa kila udhahili.
