Yuston Media
Yuston Media
February 24, 2025 at 06:10 PM
MAISHA YA ELIZA ❤️ Sehemu ya 02 Mwenzi mmoja ulipita Eliza akapona lakini Eliza alikuwa kashika mimba,, Mama yake Eliza alichanganyikiwa ,maana Eliza alikuwa anasubilia matokeo ya darasa la Saba , Eliza nae yeye alikuwa analia tu maana ile mimba ilimchanganya hakujua ataitunza vipi na utoto ule , mama yake Eliza akarudi ofisini kwa kina Baraka na kuwaambia kuwa mwanawe alivyobakwa amepewa ujauzito, kampuni ikamwita tena Baraka na kumuweka kikao na wakaamua Baraka atakatwa kila mwezi kiasi cha laki mbili atapewa Eliza mpaka atakapojifungua na labda amuoe waishi wote ,Baraka alilalamika na kuwaambia mabosi wake kiasi hicho ni kikubwa maana yeye analipwa laki tatu na nusu kwa mwezi sasa akikatwa laki mbili nzima itakuwaje ,? Mabosi wa Baraka wakamwambia Baraka wanafanya hivyo ili kuficha aibu ya kampuni yao maana mama Eliza akienda kushtaki kuwa mtoto wake kabakwa na mfanyakazi wa hapa kampuni yao itasimamishwa kazi , Baraka akakubali kukatwa laki mbili kila mwezi , Eliza akatengenezewa kikadi maalumu ikifika mwisho wa mwezi anaenda benki na kikadi hicho na atakuwa anadroo pesa kama kawaida , Baraka alikuwa mnyonge sana maana hakujua kitendo alichokifanya kingemuthiri kiasi hicho , na hakujipanga kuoa maana kwao ni mbali na hapo kijijini alikuja na hiyo kampuni ya uchongaji wa barabara, Kazi ya kuchonga barabara ikaisha na kampuni ikahama na kuhamia Rwanda Baraka nae akahama na kampuni hiyo na maisha ya Eliza yakaendelea huku akienda kudroo pesa kama kawaida , Sebastian au wanamuita Seba,kijana wa hapo kijijini kwa kina Eliza anapata taarifa kuwa Eliza japo anamimba lakini kila baada ya mwisho wa mwezi anachukua laki mbili kutoka benk za matumizi , anamuua kwenda na kuongea na mama yake Eliza kuwa anataka kumuoa Eliza aishi nae hivyo hivyo na ujauzito wake , Mama yake Eliza anakubali na mipango ikafanywa na Eliza akaolewa na Seba, Mwanzoni maisha yalikuwa mazuri sana na Seba alikuwa anakwenda kazini sasa ukichanganya kipato cha Seba na zile laki mbili za kila mwezi za Eliza mambo yalikuwa mazuri kwa upande wao , Mama yake Eliza akapata ajali gafra tu na kupoteza maisha , Eliza alilia sana na akawa hana pa kutegemea zaidi ya mumewe Seba , Lakini baada ya miezi kupita Seba alibadirika na kuwa ni mtu wa pombe , na kazini akafukuzwa akawa hana kazi wakawa wanategemea ile laki mbili ya kila mwezi , Kile kikadi akakichukua Seba na akawa anakwenda kudroo yeye pesa , sasa akitoka kudroo hupitia baa na kunywa Pombe na akirudi ni matusi mtindo mmoja ,Eliza akidai pesa anapigwa , yakawa ndio maisha ya Eliza , Miezi 9 ikafika Eliza akashikwa na uchungu akiwa ndani mumewe yuko baa anapiga mitungi , majirani wakamsaidia na kumpeleka zahanat ya kijiji ,na zahanat walimpokea lakini baada ya vipimo wakamwambia anatakiwa awaishwe hospitali ya mkoa ili aongezwe njia maana njia yake ni ndogo , Eliza kwa msaada wa majirani akapelekwa hospital na akajifungua salama ,mumewe Seba alipelekewa taarifa za mke wake lakini hakujali wala hakwenda hospital alichokifanya akamchukua mwanamke mwingine na kumuoa yaani mkewe yupo hospitali yeye huku akaoa mke mwingine, Eliza alikaa hospital wiki mbili na alijifungua salama mtoto wa kiume huku chakula akiletewa na majirani na aliporuhusiwa anarudi nyumbani anamkuta mwanamke mwingine ndani ya nyumba wanayoishi na mumewe, " "mume wangu huyu ni nani "? Eliza aliuliza , "Huyu ni mke wangu mpyaa nanaomba umuheshimu " Seba alijibu bila wasi wasi , " Lakini Seba mbona unanifanyia hivyo basi nipe ile kadi ya benki mi niende nikaishi sehemu nyingine," Eliza alilalamika na kuomba ile kadi ya benki , " Yaani wewe ungekuwa hutoki hospital ningekuzaba makofi ,yaani unadai ile kadi kwani hapa huli ,? Au nimekufukuza , yaani mi naishi nawewe tokea unamimba ya mtu mwingine mpaka umeenda kuzaa unakula na kunya kwangu bado huna shukuran,sasa kama unataka kuondoka ondoka kama utabaki baki ila kadi sikupi ," Seba aliongea na kuingia ndani , Eliza alilia sana lakini haikusaidia ,maisha yakawa magumu kwake kwani hata kulala analala sebuleni na katoto kake Seba na mkewe mwingine wanalala chumbani , ** Baraka aliendelea kufanya kazi kwa bidii huku mshahara wake ukikatwa kila mwezi yaani laki mbili zinakwenda benki na zinazobakia ndio anapewa yeye na hakuwa na namna na hakuweza kurudi kule alikomuacha Eliza , ** Pale ndani maisha ya Eliza yalikuwa magumu sana maana hata Seba akichukua pesa benki hampi anazitumia na mkewe mwingine tena baa na wakirudi wamelewa chakali , Siku moja walilewa na kile kikadi cha benki kikapotea , ITAENDELEA

Comments