
Yuston Media
February 25, 2025 at 04:53 PM
MAISHA YA ELIZA ❤️
Sehemu ya 03
Siku moja walilewa na kile kikadi cha benk kikapotea ,
Asubuhi na mapema Seba aliamka na kuanza kukitafuta kikadi hicho lakini hakukiona ,akajua Eliza ndo kakichukua , akamfuata alipolala na kumuamsha na makofi mengi , "nipe kile kikadi upesi " aliongea Seba kwa ukali ,
" Jamani baba John mimi sijachukua hicho kikadi " aliongea kwa huruma Eliza ,
"Funga bakuli lako halafu ukome kuniita baba John mimi sina mtoto nawewe " alizidi kuongea Seba ,
Eliza alishindwa kuelewa hicho kikadi kimepotea potea vip maana ndicho wanachotegemea kwenye maswala ya chakula hapo nyumbani, Seba alimpiga Eliza huku akimwambia amuoneshe kikadi hicho na Eliza hakuwa nacho ,maisha yakawa magumu kwa upande wa familia hiyo kwani Seba alikuwa anategemea hiyo laki mbili kila mwezi na maisha ya kijijini hiyo pesa ilikuwa inatosha kabisa na ndio maana akaoa na mke wa pili,
Maisha yakabadilika ikawa Eliza akawa anafanya vibarua vya kilimo na kukata kuni polini na kuuza kijijini hapo na kupata pesa kidogo , alichopata alinunua unga kidogo na kula na mwanae ,
Mke mwingine wa Seba akaona chuki akamwambia Seba kuwa Eliza anamnyima chakula , Seba akakasirika akamtukana sana Eliza na kumfukuza nyumbani hapo na kumwambia kwanza yeye alimsaidia tu kutokana na mimba yake na sio kama anampenda ,
"Mimi nilikupa msaada tu wa kuishi hapa kwa sababu ulikuwa na mimba na wala sikukupenda ondoka kwangu, unamnyima mke wangu chakula unazani mimi siwezi kutafuta "
Aliongea kwa hasira ,
" Nisamehe mume wangu mimi sina sehemu ya kwenda ntaenda wapi mimi na mtoto, " aliongea Eliza huku akitia huruma ,
" Utajua mwenyewe na ukitaka kukaa hapa kwangu basi unachopata kilete hapa nyumbani tule wote mshenzi mkubwa wewe,"
Aliongea Seba huku akikunja shati lake na kuondoka zake ,
Eliza alilia tu asijue wapi pa kuanzia na wapi ataishia ,
***
Baraka alipandishwa daraja kutoka kibarua mpaka kuajiriwa na alipoajiriwa aliongezewa mshahara na akawa analipwa laki 8 kwa mwezi lakini kutokana na ile ishu ya kum baka Eliza waajiri wake wakaamua kumpa Baraka laki tano kwa mwezi huku laki tatu ikienda kwenye ile akaunti ya Eliza bila kujua Eliza ameshapoteza kile kikadi , ile pesa ilikuwa inaongezeka kila baada ya miezi na sasa ikatimia mwaka mmoja huku akaunti hiyo ikisoma ni milioni 3 na laki 6 na baraka hakujua hilo kwa vile yeye mshahara wake hukatwa juu kwa juu ,na wale waajiri wake wakajua Eliza ameamua kuiacha pesa hiyo ili iwe nyingi na labda aje aifanyie biashara baadae kumbe Eliza anakula msoto wa nguvu na anapitia shida balaa ,
****
Eliza alikuwa anafanya vibarua huku mvua ikiwa yake na jua likiwa lake na mtoto wake ,na pesa akizipata basi huzigawa nusu anachukua Seba akanywe pombe na nyingine hupika chakula kwa ajili ya familia nzima ,yaani pamoja na mke wa Seba ,akikataa ni kipigo,
Mke wa seba yeye alikuwa hafanyi kazi alikuwa anapiga umbea tu nyumbani na Eliza huamka saa 12 na mtoto wake kwa ajili ya kusaka vibarua ,
Siku hiyo Eliza alikosa vibarua akaamua kurudi nyumbani akiwa na mwanae mgongoni kwenye kanga alikuwa na mia tano tu akaamua amnunulie mwanae ndizi za kukaanga angalau apoze njaa kwa sababu ilikuwa ni saa 8 mchana jua linawaka na hawajaweka kitu tumboni ,
Alinunua ndizi hizo na kuzibeba mpaka nyumbani na alipofika akamkuta mke mwenzake anamsubilia ,
" Yaani umeondoka hujaacha hata hela ya uji unategemea mi ntakula nini," aliongea mwanamke huyo bila hata aibu ,
Eliza hakumjibu aliingia ndani na kumuwekea mwanae ndizi kwenye sahani ili ale ,
Lakini kabla hata hajaanza kula akaingia yule mke mwenzake na kuzichukua zile ndizi na kuanza kuzila ,
"Mshenzi wewe yaani unajifanya husikii nilichokuambia sasa mi nakula hizi ndizi "
Eliza alikaa tu na kuanza kulia maana hata kupigana alikuwa hawezi ,
" Mama acha kulia mimi sina njaa "
Ilisikika sauti ya mtoto John mtoto wa Eliza baada ya kumuona mama yake akilia kwa uchungu huku akimkumbatia ,
John alimfuta mama yake machozi na mama yake akapata nguvu kidogo na kum beba mwanae na kuondoka zake kutafuta kuni ili aje aziuze apate japo kula siku ya leo ,
***
Kampuni ya Video shutting and editing limited, ilikuwa ndani ya poli ikifanya moving, muvi hiyo ilikuwa inahusu mtoto wa kijijini mwenye akili nyingi na anae pitia mateso baada ya baba yake kufariki na kuachwa na mama yake tu, walijenga vijumba kama vya kijijini na kuwaweka wahusika na mambo yakawa yanaendelea ,
Wakati wanaendelea na kushut muvi hiyo Eliza alikuwa karibu kabisa na eneo hilo alikuwa anatafuta Kuni akashangaa kusikia watu wanasema ACTION,,! ikabidi aangalie vizuri akaona kuna watu wapo bize na makamera huku kuna mtoto makamo ya mwanae anakula chakula huku camera ikielekezwa kwake ni kama alikuwa wanashuti , Eliza akamshusha mtoto wake John na kumwambia " mwanangu nenda pale kaombe chakula ule na uhakikishe unashiba kabisa sawa mwanangu, ?
John akaitikia "sawa mama"
Mhusika mkuu kwenye muvi hiyo alikuwa ni mtoto huyo alikuwa anakula chakula , mtoto huyo waliemtoa mjini ,sasa mtoto huyo alitakiwa aigize kama mtoto wa kijijini sasa kama unavyoelewa mtoto alieishi mjini hafanani na wakijijini hata kama utamfosi aigize maisha ya kijijini, kwahiyo mtoto huyo alikuwa anakula chakula kile kama hataki , "huyu mtoto katokea wapi tena jamani"? Aliuliza director wa muvi hiyo huku wasanii wengine wakishangaa tukio lile , mtoto John alisimama katikati ya mtoto yule aliekuwa anakula msosi kama hataki bila kujua mwenzake ni msanii na hapo anaigiza ,
"Naomba chakula nina njaa " aliongea John huku amemkazia macho mtoto mwenzake huyo ,
" SITAKI ,,! akajibu mtoto huyo kwa jeuri,
Mtoto John akapandwa na hasira akamkata kofi moja languvu mtoto huyo na kuchukua kile chakula na kuanza kula pale pale , tukio hilo kila mtu aliliona mpaka director wa muvi hiyo alisahau kuzima kamera na tukio hilo likajirekod na kuwa kipande kitamu sana kukitazama ,
mtoto John alipiga matonge kama matatu kisha akamwambia yule mtoto mwenzake " Asante kwa chakula ila hichi kilichobaki sikupi nampelekea mama yangu yule kulee " mtoto John aliongea huku akimnyooshea kidole mama yake na wasanii wote wakamuangalia Eliza na Eliza akaanza kutetemeka akijua mwanae amelikoroga ,
ITAENDELEA