
Yuston Media
February 27, 2025 at 05:44 PM
MAISHA YA ELIZA ❤️
Sehemu ya 05
"mmh,"!
Aliguna Baraka ,
Baraka akarudia kumuangalia tena na tena yule mtoto akagundua nikweli wamefanana sana ,akajiuliza inawezekana vipi mtoto maarufu kiasi kile afanane nae ,? Baraka hakujua kuwa mtoto yule ndio mtoto wa Eliza ambae mimba yake ilipatikana baada ya yeye kum baka , wakati anashangaa na kujiuliza simu yake ikaita na mpigaji alikuwa ni kaka yake wakuzaliwa kabisa , "wee dogo vipi mbona hujatuambia kama unamtoto,"? Aliongea kaka mtu,
"Mtoto,"? Aaah aah mi sina mbona broo ningewaambia ," alijitetea Baraka ,
" Inamaana huyu mtoto maarufu sio wako mbona kafanana nawewe ,"? Alizidi kuongea kakayake na Baraka mwenye rafudhi kama ya kizaramo ,
" Hapana broo maana hata mimi Nashangaa " aliongea Baraka ,
Wakaagana lakini bado Baraka alikuwa na mawazo sana juu ya mtoto huyo maarufu sana mjini,
Baraka alikuwa anashangaa kwa sababu yeye anamke na mtoto mmoja tena wakiume anamiaka mi tatu lakini sio mjanja kama mtoto huyo, japo mtoto wake wamefanana pia na mtoto huyu,
" au huyu ni yule mtoto wa Eliza ,? Lakini Eliza si yupo kule vijijini,? Aah huyu sio," aliwaza baraka huku akiirudia rudia kile kipande cha kuchekesha ,
" Daah ila kweli unajua kafanana na mimi yaani ningekuwa na demu mjini lazima ningesema huyu ni mwanangu hahahaaa" Baraka aliwaambia wenzake na kucheka ,
***
Kampuni ile ya filamu ilivyoona mtoto John kapata umaarufu sana na walijiingizia kipato kupitia Crip ile wakaamua sasa kuitoa na ile filamu ambayo ndio Eliza aliicheza kama mama wa mtoto John , filamu hiyo ilielezea mfalme akiwa na wake wawili na kila mke anamtoto mmoja wa kiume ,sasa mfalme akawa anampenda mke mdogo pamoja na mwanae , na mke mkubwa akawa hapendwi , ndani ya filam hiyo kuna manyanyaso chuki za wazi baina ya wake wawili na ngumi zikitembea kwa watoto hao, wote wakigombania ufalme baada ya baba yao kufariki , john anaibuka mshindi na kuwa mfalme mtoto akikiongoza kijiji kizima ,
Matangazo ya uzinduzi wa filamu hiyo yalikwenda sawa huku kwenye kava la filamu hiyo akiwekwa Eliza na mtoto wake John na yule mtoto mwingine waliocheza pamoja kipande cha mwanzo kabisa cha kichekesho,
Jiji la Dar es salaam linazizima kila mtu anahamu ya kuwaona waigizaji chipukizi waliofanya vizuri ndani ya muda mfupi tu,
Eliza na mwanae walikuwa maarufu sana kwa mjini maana jiji zima la dar es salaam hawajawahi kuwaona sasa kila mtu anahamu ya kuwaona watu hao haswa kwenye uzinduzi wa filam hiyo,
**
Baraka aliendelea kukatwa mshara wake na ndani ya miaka minne benki kukawa na milion kumi na nne na laki nne , Baraka alijua kila akikatwa pesa hizo zinachukuliwa na Eliza ,na hakujua kuwa Eliza alishapotezaga kikadi kile cha benk na hawakwenda kutoa taarifa benki, benki ilitunza pesa hizo huku ikijua labda mwenyewe aliziacha na kuziongeza ili ziwe nyingi kwa ajili ya kufanya biashara ,
****
Eliza akiwa na mwanae John hawajui kuwa wao ni watu maarufu sana ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania pia , na hakuna yeyote kwenye kijiji chao anaejua kuwa Eliza na mwanae ni watu maarufu kupita maelezo ,
Kijijini hapo kuna watu walimzarau Eliza kutokana na maisha yake ya kuokota kuni na kuuza kisha kupata pesa , kila mtu kijijini hapo hakuyaingilia maisha ya Eliza japo walijua anachofanyiwa na mumewe Seba sio kitu kizuri,
Ni miez mitano sasa imepita tokea Eliza apewe zile laki moja na wale wasanii sasa pesa hizo zilikuwa zimekwisha na siku hiyo Eliza alikuwa mgonjwa hivyo hakwenda kwenye Kuni ,alikuwa amejilaza sebuleni akiugulia maumivu ya kichwa huku mtoto wake John akiwa pembeni yake akim bembeleza mama yake apone , gafla aliingia Seba akiwa kalewa na alipoingia tu alidai chakula , Eliza akamwambia hajapika kwa sababu leo anaumwa na hakwenda kutafuta kuni , Eliza akashangaa anapokea bonge lakofi na matusi juu ya nguoni tena mbele ya mwanae John , "baba muache mama "" mtoto John aliongea huku akimng'ata Seba kwenye mkono ,
"Ntakuvunja mtoto Ms*en*ge wewe hebu niache " alitukana seba huku akimpiga kofi mtoto john na kudondoka chini,
Msafara wa magari ya kifahari tena ukiwa na afisa utamaduni Tanzania , uliingia kijijini wanapoishi Eliza na mwanae, watu waliyashangaa magari hayo kwani kila gari ilibandikwa picha ya Eliza na mwanae huku maneno yakisomeka UZINDUZI WA FILAMU ,
Magari hayo yalifunga break kwenye nyumba ya Seba na wakati huo Seba alikuwa anampiga Eliza huku akim buruza na kutoka nae nje ,
"Mshenzi wewe toka kwangu mpuuzi wewe na iwe mwisho leo kukanyaga hapa kwangu , " aliongea Seba huku akimsukumia nje Eliza na mwanae ,
nje ya nyumba hiyo kulikuwa na magari yaliyojipanga kama Saba na yote ya kifahari , watu kwenye magari hayo wote walishuka huku wakishangaa tukio lile , wanakijiji nao walikusanyika kushangaa magari hayo yaliyobandikwa sticka za Eliza na mtoto wake John , Seba nae alishangaa baada ya kumtoa Eliza nnje na kukutana na magari ya kifahari na yote yanapicha ya Eliza na mwanae John huku akiwaona watu waliokuja na magari hayo wameshuka na wote wametinga suti za maana ,
Seba Akatoa macho kama mjus kabanwa na mlango ,
ITAENDELEA
Koment yako ni muhimu 🙏🙏🙏
👍
1