
Yuston Media
February 28, 2025 at 05:35 PM
MAISHA YA ELIZA ❤️
Sehemu ya 06
Seba akatoa macho kama mjusi kabanwa na mlango,
Eliza alikuwa kaanguka chini huku mwanae John akimkumbatia akilia nayeye ,
"Nyie ni kina nani " aliuliza Seba huku akiwaangalia mmoja mmoja , hakuna mtu aliemjibu na kati kati ya magari yale akashuka Afisa utamaduni yaani yeye maswala yote ya sanaa anahusika ,
"Ndio huyu "? Afisa aliuliza huku akimwangalia Eliza maana hakutarajia anachokiona ,
"Ndio muheshimiwa na ndio maana tukasema inabidi tuje na watu wa mekap pamoja na scrab kwa sababu hawezi kwenda kwa Rais akiwa hivi,"
Seba akazidi kushangaa ( Rais anataka kumuona mke wangu mbona sielewi,) aliwaza Seba huku bado akishangaa watu wale ,
" Ok basi muandaeni kisaikorogia na wewe ni mumewe "? Aliuliza Afisa '
"Ndio mi nimumewe " alijibu Seba kwa kujiamini,
"Sasa mbona ulikuwa unampiga mkeo"? Yule Afisa aliuliza ,
"Ni mke wangu kwani we unamtaka,? kama unamtaka mchukue mi nimeshamchoka ndo maana nampiga ," aliendelea kujibu Seba ,
" Basi nikupe darasa la bule ,mke hapigwi hata kama anakosea kaa nae chini mkanye na umwambie nakupenda sana mke wangu usirudie kosa hili ," aliongea yule Afisa kwa upole lakini Seba bado alikuwa m bishi
" yaani mimi nisimpige , kwa taarifa yako mi nnamke mzuri kushinda hiyo takataka,mke wangu njoo wakuone " Seba alijitamba na yule mke wake Seba akatokea na kumkumbatia mumewe,
"Umeona chombo hiki sasa hebu muangalie huyu na huyo takataka ufananishe " bado Seba alijitamba na watu wote wakacheka ,walimcheka Seba maana hajui analolifanya ,
Afisa akamgeukia Eliza aliekuwa amekaa chini huku akijifuta machozi kwa aibu maana alikuwa anazalilishwa na Seba tena mbele ya umati wa watu ,wanakijiji wote walikusanyika kujua kulikon magari yale kuja kijijini kwao tena yakiwa na picha za Eliza ,
Eliza nae kwa upande fulani alishangaa magari yale na watu waliokuja maana magari yote yanapicha yake ye akachukulia kawaida tu,
"Hongera mwanangu tumeyaona maisha yako kabla ya kukuona mwenyewe, yaani maisha yako yameshatangulia mbele halafu wewe bado upo nyuma , binafsi sijatarajia kukuona kwenye hali hii, inashangaza sana ,hivi ninavyoongea Rais anataka kukuona sasa itabid ujiandae ," aliongea Afisa utamaduni ,
" Raisi ,"? Yaani mi nikaonane na raisi mmh" aliwaza Eliza lakini moyoni pia alishukuru kuondoka eneo hilo japo hajui huko anakokwenda atakaa wapi ,
". Heeheheeeeeeee majiranii nahukuuuuu,,vichekesho vya mwaka yaani huyu akaonane na Rais" aliongea yule mke wa Seba kwa kubeza na kubinua midomo 😏,
"Dada hujui huyu mtu anathamani gani kwa hiyo kaa kimya la sivyo ntatumia mamlaka yangu ," aliongea yule Afisa ,
Ikabid mke wa Seba akae kimya na haraka wakashuka wasichana Wazuri na kumnyanyua Eliza na vijana wawili wengine wakamshika mtoto John , wakaenda uwani kwa ajili ya maandalizi , Eliza aliwekewa waiving la garama nguo za bei mbaya ,kiatu cha kokoko, uzuri wake ukaonekana mara dufu , Eliza alikuwa mrembo sana ni zile shida tu , mtoto john nae akavalishwa nguo za kisasa na hata ukimuona huwez kumzania , walitoka kule uwani na kutokea huku mbele ambako Seba na mke wake pamoja na wanakijiji walikuwa wanawasubilia , hakuna alieamini kila mtu alitoa macho kumshangaa Eliza , Eliza alikuwa mrembo haswa alivalia gauni lefu na huku nyuma kuna warembo wawili walilishika maana lilikuwa linaburuzika chini , Eliza alitembea kwa madaha kama yupo kwenye mashindano ya urembo na kumpita Seba akiwa na mkewe , Seba hakuamini anachokiona alimwangalia tena Eliza na kuuliza " ELIZA YUPO WAPI ,"? watu wakacheka maana Eliza ndo alikuwa mbele yake ,
"Haya mfananishe tena mkeo na huyu takataka " aliongea yule Afisa na watu wote wakacheka ,
"Hapa naota au mbona sielewi " aliongea Seba baada ya kumuona mtoto john nae akitokea kule uwani,
John nae alipendeza huku akitembea kama anadunda watu wote wakacheka maana ilikuwa ni kama burudani ,
"Sasa mke wangu unaenda wapi mbona huniagi " aliongea Seba huku akimwachia yule mke wake na kumfuata Eliza , haraka mabaunsa wakamzunguuka Eliza na kumzuia Seba ,
"We mbona kigeu geu we si umesema huyu sio mkeo"? Aliuzwa Seba na yule Afisa,
""Aaah aah mimi mbona kama sijasema ," alipatwa na kigugumizi ,
"Sasa nisikilize kama ulikuwa hujui ndo nakwambia sasa yule Eliza uliekuwa unampiga na kumnyanyasa sio Eliza huyu unaemuona , Eliza huyu huruhusiwi kumshika hata gauni lake , labda yeye akuruhusu umenielewa , "?
Alisema Afisa na kuelekea kwenye gar, wakapanda wote pamoja na Eliza na mwanawe na safari ya kurudi mjini ilianza ,
Huku nyuma kila mtu alikuwa anajiuliza kivyake je Eliza kafanyaje mpaka akawa vile ,"?
" Yaani magari ya kifahari yamekuja kumchukua Eliza utazani malkia " aliongea mmoja wa wanakijiji ,
Seba ndo alikuwa na mawazo kibao hata mkewe alipomsemesha alimfokea , " unashindwa kujua Eliza amefanya tukio gani mpaka akafuatwa huku kijijini na magari?
Seba aliongea kwa ukali ,
"Lakini mume wangu punguza hasira si atarudi tutamuuliza " aliongea mkewe Seba ,
"Atarudi arudi wapi yule we jinsi ulivyomuona amebadirika vile yule sio mtu wa kurudi , nakwambia hawezi kurudi nitamfuata huko huko" aliongea Seba huku akipiga ngumi ukutani,
Magari yaliingia mjini dar es salaam, huku kila kona ya mji huo kuna matangazo ya UZINDUZI WA FILAMU yakiambatana na picha za Eliza , Eliza alishangaa sana hakujua kuwa kile kitendo cha siku ile cha kuigiza kingesababisha mambo makubwa kiasi kile,
"Mama ona picha zako na zangu ," aliongea mtoto John akishangaa matangazo ya barabarani ,
"Ndio mkuu tunakwenda ikulu au tumfikishe hotelini kwanza " aliongea dereva kwa njia ya simu ,
" Twendeni hotelini kwanza ndo tupate ratiba ya Rais " ilisikika sauti ya upande wa pili , Eliza bado alishangaa ( Rais na mimi wapi nawapi jamani ) Eliza aliwaza mwenyewe na kuona magari yakipaki nnje ya hotel ya kifahari ya gorofa,
Ile kitendo cha kushuka tu akashangaa kundi kubwa la waandishi wa habar wakimzonga kila mtu anamuuliza swali lake , mabaunsa walifanya kazi yao ya kumlinda Eliza na mwanawe,, Eliza yeye alishangaa tu umaarufu aliokuwa nao mjini wakati kijijini anateseka vibaya sana ,
Seba kitendo cha Eliza kuondoka kijijini kilimpa aibu sana siku ile ile akachukua usafiri wa basi na kwenda nayeye dar japo hajawahi kufika lakini aliamini lazima atamuona Eliza ,
"Naenda kumuharibia haiwezekani afanikiwe kirahisi vile lazima tukose wote " alisema Seba huku akikaa kwenye siti ya basi,
Je Seba atafanikiwa kumuharibia Eliza ,"?
Na Eliza ataongea nini akikutana na Rais,
Usiache kukomenti 🙏🙏
ITAENDELEA