
Yuston Media
March 1, 2025 at 03:15 PM
MAISHA YA ELIZA ❤️
Sehemu ya 07
Basi lilisonga huku likiingia jijini dare es salaam Seba akiwa kakaa siti ya dirishani akiangalia jinsi majengo makubwa na ya gorofa yalivyoupamba mji huo,
Wakati basi hilo limesimama kwenye mataa akashangaa kuona picha za Eliza na mwanae John zimebandikwa kwenye ukuta huku zile tv za barabarani nazo zikionesha matangazo hayo,
"Mmh au Eliza alikuwa jini amewezaje kuwa mtu maarufu kiasi hiki ," aliwaza Seba huku akikaza macho kuangalia tangazo lile ,
Ilipita wiki moja huku Eliza na mwanawe wakila Bata kwenye hotel ya kifahari , mala nyingi Eliza alikaa juu ya gorofa hilo nakuangalia manzari ya jiji la dar es salamu huku akiwaza mateso aliyoyapitia , " mmh ni MUNGU tu ameamua kunifanya hivi ,"alijisemea Eliza huku taratiibu akinywa juis yake ya matunda , mtoto john yeye alikuwa amekaa ndani kwenye sofa kubwa la kubembea huku akiangalia katoun yeye john hakujua kuwa maisha hayo ni yeye na mama yake ndo wamesababisha kwa kuigiza muvi ,
Walifika masponsa mbali mbali na na wasanii maarufu ,magari yalijipanga hotelini hapo huku mabaunsa wakinipanga kwa ajili ya umati wa watu kila mtu akitaka kuwaona Eliza na mwanawe John live , Eliza na mwanae walikuja kuchukuliwa ili wakakutane na Rais, katika umati huo uliosimama nje alikuwepo Seba , Seba alikuwa anashangaa na kujiuliza nini kilitokea mpaka Eliza kuwa mtu wa namna hii, mlango wa hotel ulifunguliwa kila mtu macho yakawatoka huku wakisukumana kumuona Eliza na John ,waandishi wa habari nao hawakuwa nyuma kila mtu alielekeza kamera kuchukua japo picha mbili au tatu, " mke wanguuu ,,! Ilisikika sauti ya Seba akiita baada Eliza kutoka na kusindikizwa na mabaunsa, Eliza alisikia sauti hiyo na kusimama akaangalia ilipotokea akamuona Seba akiwa kati kati ya watu akinyoosha mkono akitamani hata kumgusa japo gauni tu alilovaa ,
"Mke wangu ni mimi mumeo sebaaa " Seba aliongea huku watu wakimcheka walimuona punguani maana jinsi alivyo na jinsi alivyo Eliza ni mbingu na aldhi , Eliza alitabasamu tu na kutingisha kichwa kama anakataa na akafunguliwa mlango wa gari na akaingia na msafara ukaanza ,
Seba akaona kama amefanyiwa dharau akajisemea kimoyoni "huyu hanijui lazima nimkomeshe yaani nitahakikisha anakuwa kichaa tena atafutika kabisa mpuuuzi huyu,"
Eliza hakuamini anachokiona mbele yake alisimama Rais wa Tanzania, na waheshimiwa kibao , alianza kumsalimia kwa heshima kubwa huku machozi yanamtoka asiamini kama amekutana na Rais , Rais alimpongeza Eliza na mwanawe huku akimpakata mtoto john ,ilikuwa ni furaha , waliongea mengi ikiwemo kumshauli Eliza kutokubweteka na umaarufu aliokuwa nao pamoja na pesa atakazo pewa , "fanya kazi mwanangu Mungu amekuchagua wewe na mwanao sawa " Rais alimwambia Eliza , Eliza aliitikia na kupokea ushauli na mwisho akapewa zawadi kutoka kwa Rais na akaaga na safari ya kurudi hotelini ikaanza ,
** Wiki moja baadae **
Kilichokuwa kinasubiliwa kiliwadia huku ukumbi mzima wa sinema ukijaa watu ilikuwa ni siku ya UZINDUZI WA FILAMU na mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa utamaduni sanaa na michezo, redi kapet ikipambwa na wasanii mbali mbali wa muziki wa kizazi kipya, walianza kuingia wasanii mbali mbali walioigiza muvi ile na alipoingia Eliza na mwanae ukumbi mzima ulilipuka kwa vifijo na kelele za kushangilia ,huku Eliza akiwapungia mkono na kuwasalimia pembeni alisindikizwa na walinzi, alikaribishwa kama malkia huku John nae akipewa kiti chake , picha zilipogwa sehemu alipokaa , lakini kadri picha hizo zinavyopigwa Eliza alisikia maumivu ya kichwa , maumivu hayo yalianza taratibu na yakazidi na kuzidi , Eliza alijikaza sana lakini muda unapozid kwenda akaanza kulikunja gauni lake zuri alilovaa halafu akataka kulichana akasita , ilionekana kama hayuko sawa yaani kama mtu anaetaka kuchanganyikiwa ,
"" kwani hapa kuna nini,? Mbona kuna watu wengi " alijiuliza Eliza, alionekana tayari kumbukumbu zake zimeshaanza kupotea ,
"Mama ona zawadi zangu nimepewa " mtoto john alimwambia mama yake ,lakini badala ya mama yake kumjibu akamwambia " mwanangu twende zetu baharini tukavue samaki , " John akashangaa , " mama baharini na usiku huu"? Mtoto John aliuliza kwa mshangao, " ndio kule kuna mmbwa atatung'ata " alijibu Eliza huku akiangalia watu , watu walikuwa bize na sherehe ile na hawakuweza kusikia kama Eliza anaropoka maana kulikuwa na sauti kubwa ya mziki ,
Eliza akamshika mwanae mkono tena kwa nguvu kisha akamwambia " mwanangu siwezi kukuacha hapa polini uliwe na simba , " Eliza aliongea huku akisimama na kukishika kile kiti cha chuma halafu akaangalia kule kwenye sinema nia yake akirushe kile kiti kule kwenye sinema ili aharibu kila kitu,
John akashangaa na kujiuliza mama yake amepatwa na nini ,?
Nini kitatokea ukumbini hapo ?
Na je Seba ndo kashafanya yake ,?
Usikose kusoma story hii ya kusisimua,
Like na koment 🙏 tu ili tujue tuko wangapi kwenye story hii,