
Aviation Media Tanzania
February 5, 2025 at 06:23 AM
Katika ziara yake ya kiwanja cha ndege cha Mtwara, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Ludovick Nduhiye amepongeza maendeleo yaliyofanyika
katika kiwanja hicho ikiwa ni pamoja na uwezo wa
kiwanja hicho kufanya kazi saa 24, huku akisisitiza
kuwepo kwa jitihada za makusudi ili kuvutia abiria
ili kuongeza miruko zaidi.
Meneja wa kiwanja hicho Jordan Mchami amesema
kiwanja hicho kina uwezo wa kuhudumia ndege
wakati wa usiku pamoja na wakati wa hali
inayosababisha uoni hafifu na hii ni kutokana na
kuwepo kwa taa za kuongozea ndege.
Mchami amesema; katika awamu ya kwanza
ya uboreshaji na upanuzi wa kiwanja hicho, serikali
imejenga Njia ya kurukia ndege
yenye urefu wa mita 2800 na upana wa mita 45
kwa kiwango cha lami.
Pia amesema kuwa wamefanikiwa kujenga eneo la
maegesho ya ndege, barabara ya kiungio (Taxiway)
yenye urefu wa mita 467 pamoja na ujenzi wa
barabara mpya ya magari kuingia uwanjani hapo.
