
Aviation Media Tanzania
403 subscribers
About Aviation Media Tanzania
Kwa habari za Matukio, Elimu na Burudani katika sekta ya Usafiri wa Anga.
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Mara nyingine mafunzo ya kutua helikopta juu ya meli Baharini, hufanyika nchi kavu katika mtambo maalumu unaoigilizia hali ya Meli inapokuwa kwenye mawimbi ya bahari. Mtambo huu unaweza kujongea chini, Juu, kuinama upande na hata kusogea kulia, kushoto, mbele na nyuma.


Je, unaweza kutambua kiwanja hiki cha ndege kinapatikana Mkoa gani? 📸 Auric Air Services Ltd Tanzania


Je, ungechagua kuketi wapi kati ya kiti hiki cha ubavuni na viti vya kati?


Shirika la ndege la United Airlines imefikisha ndege 1,000 baada ya kupokea Boeing 737-9 MAX (N77584) na kulifanya shirika hilo kuongoza ulimwenguni. Mashirika yanayofuata kuwa na ndege nyingi ni Delta Airlines likiwa na ndege 985 na American Airlines, ndege 978.


Ndegenyuki (Drone) ni ndege isiyo na rubani inayoongozwa na mtu au ngamizi kutoka eneo la mbali na zimegawinyika kwa 'aina' kulingana na mfumo wa uendeshaji mfano, yenye panga nyingi (multi rotor), yenye mabawa (Fixed wing) n.k Lakini pia zimegawanyika kwenye 'makundi' kulingana na uzito (#Micro, #Small, #Medium na #Large) pasipo kuangalia shughuli iliyoumbiwa. 'Drones' kiujumla zina matumizi mengi mfano, Kufanya tafiti, Kutafuta na kuokoa, Doria, kusafirisha mizigo au watu, kupiga picha, ujasusi, shughuli za kijeshi n.k 'Drone' nyingi maarufu zilizoenea zaidi ni zile ndogo za upigaji picha (Small/Camera Drone). Kwa nchi nyingi uendeshaji wa ndege zisizo na rubani 'Drone' umewekwa kisheria. Kwa hapa nchini kulingana na kanuni ya 2018 ya Usafiri wa Anga (Remotely Piloted Aircraft Systems) inamtaja mwendeshaji wa 'Drone' kama Rubani hivyo kuna umuhimu wa kupata mafunzo na leseni ya kuendesha ndege hizo. Katika mafunzo hujumuisha nadharia ya kufahamu sheria za Usafiri wa Anga, lakini pia uwezo, kanuni za uendeshaji, mfumo unaowezesha kupaa, Hali ya hewa na athari, mawasiliano ya sauti, taratibu za kufunga mizigo ya drone n.k Baada ya kumaliza mafunzo washiriki hupata vyeti ambavyo vitatumika kupata leseni ya urubani wa ndegenyuki kutoka kwa mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Kumbuka, Drone au Ndege-Nyuki zimeingizwa kwenye udhibiti wa mamlaka mbalimbali za Usafiri wa Anga ulimwenguni kutokana na muingiliano wa moja kwa moja wa matumizi ya anga na usalama wake. Mnamo mwaka 2024, tishio la kuonekana kwa 'Drone' katika maeneo viwanja vya ndege mbalimbali ulimwenguni ilipelekea kufungwa kwa muda baadhi ya viwanja vya ndege vya kimataifa kama #Frankfurt, #Dublin na #Heathrow. Lakini tukio kubwa zaidi ni kufungwa uwanja wa ndege wa kimataifa #Gatwick Uingereza kwa saa 36 na kusababisha hasara ya pauni milioni 1.4 Ndege-Nyuki 'Drone' inaweza kuwa tishio la usalama ikiwa mikononi mwa mtu asiyefahamu taratibu za uendeshaji au mtu mwenye nia tofauti. 'Drone' inaweza kusababisha matatizo kama ikiingia kwenye injini ya ndege. Lakini pia inaweza kuchanganya signal za mawasiliano, kufanya hujuma mfano kubeba vilipuzi, hewa ya sumu, kusambaza ugonjwa au hata kuvunja haki za uhuru wa kibinaadamu. Hii ni sehemu tu ya sababu kwanini 'Drones' zinahitaji kusajiliwa na kutolewa mafunzo ya uendeshaji. Kwa hapa nchini Tanzania, unaweza kupata huduma ya mafunzo ya 'Ndegenyuki' kupitia Chuo cha Usafiri wa Anga maarufu Civil Aviation Training Centre (CATC) kilichopo kwenye Jengo namba moja (Terminal One) kwenye ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere. Au unaweza kuwasiliana nao kupitia; 0752 048 002 0715 544 145


#Deicing ni mchakato muhimu wa kuondoa theluji/barafu kutoka kwenye uso wa ndege katika mikoa ya baridi kali. Katika hali hiyo, ndege ikiwa chini maegesho hupuliziwa kimiminika maalum kiitwacho 'Deicing fluid' ambacho ni mchanganyiko wa kemikali inayoitwa glycol na maji. Kimiminika hiki kwa ujumla hupashwa moto na kunyunyiziwa sehemu zote muhimu kwenye ndege ili kuondoa barafu na theluji iliyoganda au inayoanza kuganda. Ndege nyingi pia zina mifumo yake wa ndani ya kuengua au kuzuia theluji kuganda katika sehemu zake muhimu (Anti-icing) Ndege zimeundwa ili kuruka zikiwa na nyuso safi (Soft Surface Skin) na katika vipindi vya baridi, barafu zinaweza kujikusanya, kuharibu mtiririko safi wa hewa (Smooth Air flow) na kuvuruga ufanisi wa kupaa. Muhimu zaidi, sheria nyingi za usafiri wa anga zinataja kuwa, mabawa na mkia wa ndege visiwe na theluji au barafu kabla ya kupaa. Barafu iliyoganda ni hatari kwa sababu inabadilisha umbo na umbile la bawa. Mabawa uhitaji kuwa safi kwa utendaji fanisi. Theluji inabadilisha sura ya bawa (Rough Wing aerodynamic) hivyo kuvuruga mtiririko safi wa hewa ambao ndiyo chanzo cha ndege kupaa. Bawa zilizochafuliwa kwa theluji iliyoganda, hewa inashindwa kushikamana vizuri na uso wa bawa hivyo hutengana na kuleta msukosuko (Turbulent Flow). Hali hii ikitokea, ndege hupoteza lifti ambayo inaweza kuwa hatari. Hali hii usichanganye na ile kunyunyiziwa maji wakati ndege imetua. Ni desturi inayojulikana kama saluti ya maji (water salute) ambayo hufanywa kwa madhumuni ya kutoa heshima ya sherehe, kama vile wakati ndege inastaafu, Rubani kustaafu, kuzindua ndege au safari mpya. 'Water salute' pia inaweza kufanywa kama heshima ya mwisho kwa wafanyakazi wa anga au askari waliouawa katika harakati au matukio mengine mashuhuri. Admin, Aviation Media Tz


Ndege kubwa ya China ya Amphibious - AG600 imekamilisha majaribio yote ya kuruka ili kuthibitisha ustahiki wake wa anga hadi kufikia Ijumaa ya leo, na kuweza kutii mahitaji yote ya uidhinishaji wa kustahiki kutoa huduma ya anga. Familia ya AG600 yenye uwezo wa kutumika kwenye Maji na nchi kavu, inakuwa ndege kubwa ya Uchina yenye madhumuni maalum, na inatarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa robo ya kwanza ya mwaka huu baada ya kukamilisha majaribio kadhaa machache ya kimipango.


Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania imetia saini mkataba na Kampuni ya Saba Engineering Private Company Limited kwa ajili ya huduma za ushauri na ubunifu wa kina wa ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege cha kimataifa cha Serengeti. Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu huku ikishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Maulid Madeni, Menejimenti ya TAA na Mwenyekiti wa kamati ya Serengeti ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Serengeti Dkt. Rhimo Nyansaho. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Abdul Mambokaleo alielezea kuwa mradi utatekelezwa na Mhandisi Mshauri, Saba Engineering Private Company ltd kwa ushirikiano na Intairplan GMBH na Projectplus Consult (T) LTD ambapo gharama za mradi huu ni kiasi cha Shilingi Bilioni 1.3 huku muda wa utekelezaji wa mkataba utakuwa ni wa Miezi sita (6) mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huu. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Maulid Madeni amesema, kuja kukamilika kwa mradi wa kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Serengeti kitawezesha watalii kuongezeka kutemebelea mbuga ya Serengeti kutokana na urahisi wa kufika mbugani moja kwa moja pia na kuwezesha kuongezeka kwa huduma mbalimbali Wilayani Serengeti ikiwemo kodi jambo ambalo litasababisha kuongeza uchumi na ajira katika eneo hilo. Naye Mwenyekiti wa Kamati Serengeti na Mjumbe wa Bodi ya TANAPA Dkt. Rhimo Nyansaho amesema ukamilikaji wa Kiwanja cha Serengeti utawezesha urahisi wa mtalii kufika katika eneo hilo na kupunguza vikwazo vitakavyo mfanya aishie nchi jirani bila kufika nchini.


. Jumla ya washiriki 25 wamehitimu mafunzo maalumu katika Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga Tanzania (CATC). Kati ya hao, wanafunzi 19 walihitimu kutoka Kozi za Urubani wa Ndegenyuki (Ndege zisizo na rubani) huku 06 wakikamilisha Kozi ya Udhibiti wa Viwanja vya ndege (Aerodrome Control). Hafla hiyo ya kufunga rasmi iliongozwa na Mkuu wa Mafunzo wa CATC, Didacus Mweya, ambaye aliwapongeza wahitimu hao na kuwataka kulinda heshima ya taasisi hiyo kwa weledi na ubora. @catc


Ndege zilizobeba viongozi wa Nchi mbalimbali zimeendelea kuwasili kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika leo. Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
