
Aviation Media Tanzania
February 5, 2025 at 07:05 AM
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dk. Stergomena Lawrence Tax (Mb) jana amepokea ndege ya kijeshi kutoka Jeshi la Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Falme za Kiarabu.
Ndege hiyo yenye muonekano kati ya CN-235 au C-295 zinazoundwa na Airbus, awali ikijulikana kama (CASA), katika kategoria ya 'Military Cargo Aircraft' itatumika katika shughuli za kusafirishia viongozi wa kiraia na kiserikali, usafirishaji wa kijeshi, pamoja na kudondosha askari wa miamvuli.

👍
1