Aviation Media Tanzania
Aviation Media Tanzania
February 7, 2025 at 02:48 AM
Ndege wawili aina ya Swan waliigonga ndege ya Tui na kutoboa 'fuselage' na kusababisha kutua kwa dharura. Mgongono huo katika kasi ya 297km/saa, ulisababisha kupasuka kwa kioo cha mbele, na kutoboa mfuniko wa mkandamizo wa hewa na kuwazuia marubani kushinikiza ndege. Ndege hiyo aina ya Boeing 737 Max inayoendeshwa na shirika la Tui, ilikuwa imepanda futi 1,000 juu ya Gatwick kuelekea Cape Verde kabla rubani hajatangaza dharura. Baada ya kutua, Ndege ilihitaji kusindikizwa kutoka kwenye njia ya kurukia kuelekea maegesho kwani marubani hawakuweza kuona nje kwasababu ya nyufa na damu kwenye kioo.

Comments