Aviation Media Tanzania
February 7, 2025 at 03:17 PM
Ndege nyingi hufikia kikomo cha kutoa huduma au kustaafishwa "retired" kwa kufikia kiwango cha juu kwenye;
> Kuruka na kutua mara nyingi "Landing Cycle"
> Idadi kubwa ya mzunguko wa hewa yenye shinikikizo ndani ya ndege "Cabin Pressurization Cycle"
> Gharama kubwa za uendeshaji "High Operational Cost" pia
> Uharibifu au Ajali mbaya "Severe Damage" n.k
Mara nyingi umri wa matumizi ya ndege mpya toka kiwandani huwa kati ya miaka 20 hadi 25, laki pia hutrgemea na aina ya matumizi.
Baada ya hapo inatajwa kuwa, ndege sio salama kupaa kwasababu malighafi zilizotumika kutengengeza ndege husika hupoteza nguvu ya asili (metal/fibre fatigue).
Muda wa kustaafishwa ndege unapowasili, hubomolewa au kupelekwa katika eneo maalumu la hifadhi ambapo inaweza kuwa, makumbusho, ndani ya bahari kwaajili ya utalii au 'ecosystem' au kwenye makaburi ya ndege maarufu "Aircraft Graveyard" au "Boneyard"
"Aircraft Graveyard au Boneyard" ni vituo vya kuhifadhi ndege zilizostaafu na mara nyingi huwa maeneo yenye unyevu mdogo kama jangwani ili kuzuia kutu.
Hapo ndege zitakuwa zikitolewa vipuri kwaajili ya ndege nyingine, au kurejelezwa (recycle)
Baadhi hununua ndege nzima nzima kwa matumizi ya kutengeneza hoteli, migahawa, nyumba za kulala au kivutio cha utalii.
Ndege inapotoa huduma nje ya mipaka ya muda ya mtengenezaji inaweza kuleta madhara mabaya muda wowote.
Kudhibiti hilo, ndipo Mamlaka za nchi zinazosimamia usafiri wa anga ikiwemo kuangalia ubora na usalama (airworthiness) zinafanya kazi yake.
Mfano, kwa Tanzania ipo mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA).
Baadhi ya mashirika au kampuni za ndege huuza au kubadili ndege zilizokaribia kuisha muda wa matumizi kuwa za mizigo.
Si ajabu kukuta baadhi ya ndege zinafika hadi miaka 40 hadi 50 ya kutoa huduma lakini hii hutegemea na umuhimu, aina ya ndege, matumizi au sheria duni za mdhibiti.
Kwa upande wa jeshi, baadhi ya ndege huifadhiwa kwa matumizi ya baadae kama vilengeo vya shabaha, kufundishia au maonesho.
Makaburi au hifadhi za ndege maarufu zinapatikana Marekani, Canada, Urusi, Australia n.k
"Alpha Mike Tango"
👍
1