
Aviation Media Tanzania
February 9, 2025 at 04:09 PM
Ni nini haswa kinachoifanya ndege ya F-35 kuwa ya kipekee duniani?
Haionekani kirahisi na maadui.
Wakati ndege ya F-35 inaposhiriki katika mazoezi, kawaida huzishinda ndege za adui kwa kiwango cha 20 kwa 1.
Ingefanya vivyo hivyo wakati wa vita dhidi ya wanajeshi wa Urusi au Wachina, kwa sababu iliundwa kunyonya au kupotosha nishati ya rada, kwa hivyo marubani wa ndege za adui hawawezi kuiona kabla haijashambulia.
Kwa kuongezea, F-35 ina mfumo wa hali ya juu ambao unadanganya au kukandamiza rada za adui, angani na ardhini.
(Radar jamming)
Rada hizo zinaweza kugundua kitu kwa mbali, lakini haziwezi kuifuatilia au kuishambulia F-35.
Pia, injini ya ndege hiyo ina uwezo wa kupunguza joto kabla ya makombora yanayotafuta joto kuishambulia.
Ni zaidi ya ndege ya kivita.
F-35 sio tu ndege ya kupambana bali pia ni ndege inayoweza kuishi muda mrefu kuwahi kuundwa.
Katika jukumu lake, ina uwezo wa kusafisha anga za ndege za maadui ambazo zinatishia majeshi ya Marekani.
Vilevile inaweza kushambulia na kuangamiza maeneo yanayolengwa ardhini, au baharini kwa kutumia mabomu na makombora tofauti..
Sensa zake
Lakini huo ni mwanzo tu. Sensa za ndani za F-35 zinaweza kukusanya na kusambaza habari za ujasusi katika maeneo mbalimbali.
Mfumo wake wa kuweza kuzuia mifumo ya ndege nyengine pamoja na vifaa vyake vya mashambulizi angani inaifanya ndege hiyo kuwa bora dhidi ya ndege nyengine za kivita.
Kwa F-35B, ina uwezo wa kupaa angani wima na kuweza kutua mahali popote ambapo wanamaji watataka huku ikiwa na uwezo wa kubeba silaha za nyuklia ili kutoa ulinzi.
Credit:
#bbcswahili

👍
2