
Aviation Media Tanzania
February 13, 2025 at 07:12 AM
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inapenda kuujulisha Umma kuwa inarejesha
safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Iringa kuanzia Jumamosi, 22 Februari 2025.
Safari ya kwanza itaanza saa 3:00 asubuhi kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na itachukua takribani dakika 60 kufika Uwanja wa
Ndege wa Iringa.
ATCL itaanza na safari 03 kwa wiki; Jumatatu, Jumatano na
ljumaa ikitumia ndege yake, DHC-8 Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 06 katika
Daraja la Biashara na abiria 70 katika Daraja la Kawaida.
Nauli ya kwenda na kurudi ni TZS 199,200/= ikijumuisha mzigo wa hadi kilo 23, Begi la mkononi lisilozidi kilo 07 pamoja na viburidisho ndani ya ndege bila malipo ya ziada.
Aidha, Wanachama wa Twiga Miles wataweza kulipia tiketi kwa kutumia pointi zao, huku wasafiri wapya wakipata zawadi ya pointi 3,000 wanapojiandikisha kupitia Air Tanzania Mobile App.
Mteja ataweza kukata tiketi kupitia tovuti: www.airtanzania.co.tz, Aplikesheni ya
Simu ya Air Tanzania, Kituo cha Huduma kwa Wateja (+255748773900) au Ofisi
za ATCL.
Kurejeshwa kwa safari hizi kunalenga kuboresha muunganiko wa safari kwa wafanyabiashara, watali, wakazi wa lringa na wasafirishaji mizigo hivyo kufungua fursa zaidi za kibiashara na maendeleo katika mkoa huo na maeneo jirani.
