Aviation Media Tanzania
Aviation Media Tanzania
February 13, 2025 at 08:19 AM
Siku chache zilizopita, baadhi ya watu walishangaa kuona ndege isiyokuwa na muundo wa kawaida kuelekea kutua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyere. Chombo hiko kilikuwa ni "Helikopta-Ndege" ya kijeshi aina ya Bell Boeing V-22 Osprey au MV-22 Osprey (Marine Corps Variants) ni ndege inayotoa huduma mchanganyiko ya pamoja kwa misheni mbalimbali. V-22 ilianza kuzalishwa rasmi Februari 2007 ili kuchukua nafasi ya Boeing Vertol CH-46 (Chinook). Ndege hii ilitua hapa nchini Tanzania kwa ajili ya mazoezi ya kijeshi yaitwayo Justified Accord 2025, yaliyoshirikisha majeshi ya nchi kavu ya Marekani na Tanzania kwa mafunzo ya pamoja ya Operesheni za Usaidizi wa Amani. Ndege hii ya MV-22 ina uwezo wa kuruka na kutua wima kama Helikopta ya kawaida, lakini ikiwa na sifa ya ziada ya kuweza kuinamisha injini zake mbele (Tilt Rotor) na kutumia mabawa yake kupaa kwa kasi na kwenda masafa ya mbali zaidi kama ilivyo ndege za kawaida za mapangaboi (Turboprops). Sifa hii ni faida ya ziada dhidi ya Helikopta za kawaida za kijeshi ambazo hazina kasi kubwa na masafa marefu. MV-22 inaweza kubeba wanajeshi 24 wenye vifaa vya kupambana na kuruka kutoka kwenye meli au fukwe na sehemu nyingine ngumu kufikika. Inaweza kubeba mzigo wa nje "External Load" hadi Tani 4.5, kwenda umbali wa kilomita 4,100, Kujaza mafuta Angani (Aerial Refueling), kukimbia kasi ya 470-500 km/saa na kupanda usawa wa futi 23,000 - 25,000, kwa mujibu wa taarifa zinazopatikana.
Image from Aviation Media Tanzania: Siku chache zilizopita, baadhi ya watu walishangaa kuona ndege isiyoku...
👍 1

Comments