
Aviation Media Tanzania
February 22, 2025 at 08:11 AM
"Mradi huu ulisainiwa mwaka 2017 tulipambana mradi uanze lakini kwa sababu mbalimbali ulishindikana, Niliporudi kwenye wizara mwaka 2022 Rais akanipa maelekeza mahsusi kuhakikisha mradi huu unaouhusisha viwanja vya Shinyanga, Katavi, Kigoma na Tabora unaanza,"
Waziri Mbarawa ameyasema hayo juzi alipotembelea kiwanja Shinyanga kwa lengo la kuangalia maendeleo ya mradi wa ujenzi ulioanza mwanzoni mwa mwaka 2023.
Prof. Mbarawa amewapongeza wakandarasi wa viwanja vyote vinne kwa kuvumilia tangu mwaka 2017 mkataba uliposainiwa licha ya kuchelewa kwa kiasi hicho lakini bado wamekuwepo isipokuwa mkandarasi mmoja wa kiwanja cha Katavi.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Lugano Mwinuka amesema kuwa shughuli za uendeshaji wa kiwanja hicho zimesitishwa ili kupisha kazi ya ujenzi inayoendelea inayohusisha ujenzi wa njia ya kuruka
na kutua ndege, maingilio ya njia za ndege (Taxiway), maegesho ya ndege (Apron) jengo la abiria, taa za kuongozea ndege na uzio wa kuzunguka kiwanja hicho.

👍
2