Aviation Media Tanzania
Aviation Media Tanzania
February 22, 2025 at 04:57 PM
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Uangalizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Afrika Mashariki (CASSOA), Salim Msangi, amehudhuria uzinduzi wa Kituo cha Tiba ya Usafiri wa Anga (CAM). Bw.Msangi amesisitiza juu ya umuhimu wa CAM katika kuziba mapengo yaliyopo kwenye maeneo ya tiba ya usafiri wa anga na utendaji wa binadamu katika sekta ya usafiri wa anga. Alibainisha kuwa kituo hicho kitaboresha tathmini za tiba ya usafiri wa anga, usimamizi wa usalama, na uchunguzi wa ajali, kuhakikisha kuwa viwango vya kimataifa vya tiba ya usafiri wa anga vinazingatiwa. Hafla hiyo, iliyofanyika katika Makao Makuu ya CAM katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), iliongozwa na Katibu wa Mkuu kutoka Idara ya Usafirishaji nchini Kenya, Bw. Mohamed Daghar.
Image from Aviation Media Tanzania: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Mjumb...

Comments