Aviation Media Tanzania
Aviation Media Tanzania
February 26, 2025 at 05:58 PM
Wakazi wa Kata ya Kipunguni Wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es Salaam, wameanza kulipwa fidia kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere. Malipo hayo ya fidia yamezinduliwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Abdul Mombokaleo katika Mkutano wake na Waandishi wa habari uliofanyika ndani ya ukumbi wa Ofisi za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Akikabidhi Hundi ya Bilioni Ishirini kwa kiongozi wa serikali ya Mtaa mbele ya Mbunge wa Segerea, Mhe. Bonnah Kamoli, Mambokaleo amesema kuwa, huo ni mwanzo tu katika mchakato endelevu wa kulipa fidia kwa wakazi hao wa Kipunguni unaofanywa na serikali ya awamu ya sita. https://youtu.be/7yBOEqvSgbA?si=SxSQtNt2DXkPz84z
👍 😂 2

Comments