
Aviation Media Tanzania
February 27, 2025 at 05:10 PM
Ndegenyuki (Drone) ni ndege isiyo na rubani inayoongozwa na mtu au ngamizi kutoka eneo la mbali na zimegawinyika kwa 'aina' kulingana na mfumo wa uendeshaji mfano, yenye panga nyingi (multi rotor), yenye mabawa (Fixed wing) n.k
Lakini pia zimegawanyika kwenye 'makundi' kulingana na uzito (#micro, #small, #medium na #large) pasipo kuangalia shughuli iliyoumbiwa.
'Drones' kiujumla zina matumizi mengi mfano, Kufanya tafiti, Kutafuta na kuokoa, Doria, kusafirisha mizigo au watu, kupiga picha, ujasusi, shughuli za kijeshi n.k
'Drone' nyingi maarufu zilizoenea zaidi ni zile ndogo za upigaji picha (Small/Camera Drone).
Kwa nchi nyingi uendeshaji wa ndege zisizo na rubani 'Drone' umewekwa kisheria.
Kwa hapa nchini kulingana na kanuni ya 2018 ya Usafiri wa Anga (Remotely Piloted Aircraft Systems) inamtaja mwendeshaji wa 'Drone' kama Rubani hivyo kuna umuhimu wa kupata mafunzo na leseni ya kuendesha ndege hizo.
Katika mafunzo hujumuisha nadharia ya kufahamu sheria za Usafiri wa Anga, lakini pia uwezo, kanuni za uendeshaji, mfumo unaowezesha kupaa, Hali ya hewa na athari, mawasiliano ya sauti, taratibu za kufunga mizigo ya drone n.k
Baada ya kumaliza mafunzo washiriki hupata vyeti ambavyo vitatumika kupata leseni ya urubani wa ndegenyuki kutoka kwa mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)
Kumbuka, Drone au Ndege-Nyuki zimeingizwa kwenye udhibiti wa mamlaka mbalimbali za Usafiri wa Anga ulimwenguni kutokana na muingiliano wa moja kwa moja wa matumizi ya anga na usalama wake.
Mnamo mwaka 2024, tishio la kuonekana kwa 'Drone' katika maeneo viwanja vya ndege mbalimbali ulimwenguni ilipelekea kufungwa kwa muda baadhi ya viwanja vya ndege vya kimataifa kama #frankfurt, #dublin na #heathrow.
Lakini tukio kubwa zaidi ni kufungwa uwanja wa ndege wa kimataifa #gatwick Uingereza kwa saa 36 na kusababisha hasara ya pauni milioni 1.4
Ndege-Nyuki 'Drone' inaweza kuwa tishio la usalama ikiwa mikononi mwa mtu asiyefahamu taratibu za uendeshaji au mtu mwenye nia tofauti.
'Drone' inaweza kusababisha matatizo kama ikiingia kwenye injini ya ndege.
Lakini pia inaweza kuchanganya signal za mawasiliano, kufanya hujuma mfano kubeba vilipuzi, hewa ya sumu, kusambaza ugonjwa au hata kuvunja haki za uhuru wa kibinaadamu.
Hii ni sehemu tu ya sababu kwanini 'Drones' zinahitaji kusajiliwa na kutolewa mafunzo ya uendeshaji.
Kwa hapa nchini Tanzania, unaweza kupata huduma ya mafunzo ya 'Ndegenyuki' kupitia Chuo cha Usafiri wa Anga maarufu Civil Aviation Training Centre (CATC) kilichopo kwenye Jengo namba moja (Terminal One) kwenye ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Au unaweza kuwasiliana nao kupitia;
0752 048 002
0715 544 145
