Aviation Media Tanzania
Aviation Media Tanzania
March 1, 2025 at 08:05 AM
#deicing ni mchakato muhimu wa kuondoa theluji/barafu kutoka kwenye uso wa ndege katika mikoa ya baridi kali. Katika hali hiyo, ndege ikiwa chini maegesho hupuliziwa kimiminika maalum kiitwacho 'Deicing fluid' ambacho ni mchanganyiko wa kemikali inayoitwa glycol na maji. Kimiminika hiki kwa ujumla hupashwa moto na kunyunyiziwa sehemu zote muhimu kwenye ndege ili kuondoa barafu na theluji iliyoganda au inayoanza kuganda. Ndege nyingi pia zina mifumo yake wa ndani ya kuengua au kuzuia theluji kuganda katika sehemu zake muhimu (Anti-icing) Ndege zimeundwa ili kuruka zikiwa na nyuso safi (Soft Surface Skin) na katika vipindi vya baridi, barafu zinaweza kujikusanya, kuharibu mtiririko safi wa hewa (Smooth Air flow) na kuvuruga ufanisi wa kupaa. Muhimu zaidi, sheria nyingi za usafiri wa anga zinataja kuwa, mabawa na mkia wa ndege visiwe na theluji au barafu kabla ya kupaa. Barafu iliyoganda ni hatari kwa sababu inabadilisha umbo na umbile la bawa. Mabawa uhitaji kuwa safi kwa utendaji fanisi. Theluji inabadilisha sura ya bawa (Rough Wing aerodynamic) hivyo kuvuruga mtiririko safi wa hewa ambao ndiyo chanzo cha ndege kupaa. Bawa zilizochafuliwa kwa theluji iliyoganda, hewa inashindwa kushikamana vizuri na uso wa bawa hivyo hutengana na kuleta msukosuko (Turbulent Flow). Hali hii ikitokea, ndege hupoteza lifti ambayo inaweza kuwa hatari. Hali hii usichanganye na ile kunyunyiziwa maji wakati ndege imetua. Ni desturi inayojulikana kama saluti ya maji (water salute) ambayo hufanywa kwa madhumuni ya kutoa heshima ya sherehe, kama vile wakati ndege inastaafu, Rubani kustaafu, kuzindua ndege au safari mpya. 'Water salute' pia inaweza kufanywa kama heshima ya mwisho kwa wafanyakazi wa anga au askari waliouawa katika harakati au matukio mengine mashuhuri. Admin, Aviation Media Tz
Image from Aviation Media Tanzania: <a class="text-blue-500 hover:underline cursor-pointer" href="/hashtag...

Comments