
DIRA LEO
January 31, 2025 at 05:41 AM
Msemo huu umekuwa ukitumika na jamii ya wazungumza Kiswahili. Hata hivyo, umekuwa ukitumika kimazoea tu ikiwa ni kama kawaida ya jamii kurithi tamaduni pasi na kuuliza mzizi wake.
Dira Leo tumejaribu kutafuta chanzo na asili ya msemo huu ili kuweza kufahamu kina na dhati yake.
Pamoja na jitihada zetu, hatukufanikiwa kupata hakika hasa ya msemo huu kutokana na kutokuwepo na chanzo cha uhakika kuhusu msemo huu.
Hata hivyo, tumepata baadhi ya hadithi zinazojaribu kueleza kuhusu msemo huu lakini hazijathibiti kama ndizo hakika ya msemo huu ama la.