
DIRA LEO
132 subscribers
About DIRA LEO
Ni Channel inayojishughulisha na Masuala mbalimbali ya kijamii yanayowahusu Watoto ,Vijana na Wazee. Imejikita katika kutoa uelewa kwa jamii Juu ya masuala mbalimbali yanayotokea katika Jamii yetu.
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Kiujumla, msemo huu kutokana na udadisi uliofanywa na Dira Leo, umekuwa ni miongoni mwa misemo yenye mabunio na makisio mengi kuhusu asili na chanzo cha kutumika kwake. Hat hivyo, Dira Leo tumejaribu kuuchimba ukweli na kuzilinganisha simulizi tofauti zilizotolewa na wadau, na tumebaini kufanana kwa namna moja ama nyingine ya visa vyote vilivyotolewa na wadau. Hivyo tunahitimisha kwa kusema kwamba, msemo huu una nasaba na utendaji usio na umakini wenye kuchochea matokeo hasi au kuleta madhara. Dira Leo tunatoa hadhari kwamba "Tuwe Makini, tusije kupata Cha Mtema Kuni" 👋

Kipi kinamfanya mtu kuwa tajiri? Leo saa 3:00 Asubuhi. Hapahapa_DiraLeo

Mdau mwingine @Kipala yeye alikuwa na haya: Lugha ninayojua ni "akifanya hivyo atakiona cha mtemakuni". Ninaelewa ni kama tishio au onyo: akifanya kitu kisicho halali ataona matokeo yake yaani atapata adhabu. Mtemakuni (pia: mtema-kuni au mtema kuni) ni mtu anayepasua miti kuwa kuni. Kwa hiyo ana kazi nzitonzito pia ni watu wenye nguvu ya kimwili. Maana neno "kutema" hupatikana kwa maana mawili moja ni "kutema mate" mengine ni "kupasua kitu" kama ubao, miwa n.k. Sina uhakika juu ya asili ya usemi lakini nimeielewa hivyo: Hawa watemakuni ni watu wenye nguvu wanajua kuadhibu. Ukitaka kuiba kwao utaona jinsi gani wanavyoweza kujitetea. - au labda pia: Watemakuni ni watu wanaoishi katika mazingira magumu msituni wakifanya kazi hii nzito heri usijaribu kucheza nao...

Mwisho tulimnukuu Mdau @Babuyao: Mtemakuni hakika ni mpasuaji au mkataji wa kuni kama wengine walivyosema. Hadithi ya mkatakuni wengine wanasema wakati akikata kuni alikosea mahesabu (umakini)shoka likatua kwenye mguu likampasua na kumjeruhi sana. Kwa hiyo, kukiona cha mtemakuni ina maana ya kujiingiza kwenye shida ya kujitakia, ni kukosa umakini katika kutenda jambo ambapo baadaye mtu anakuja kujuta kutokana na shida atakayoipata. Kumbe, ni msemo wa onyo, wa kumtaka mtu awe mwangalifu ili mabaya yasimkute. Ni msemo unaotaka seriousness ya mtu katika kutenda ili kujiepusha na matokeo mabaya.

Mdau mwingine ni @Kwetunikwetu ambaye alisema: Mimi hili nilipata simulizi toka kwa jamaa mmoja wa Kenya ambae anasema kuna mwalimu aliwasimulia shule ya msingi juu ya kisa cha mtema kuni. Hiyo hadithi inasema hivi: Siku moja jamaa mtema (mkata) kuni alienda porini kukata kuni. Sasa akakuta mti mkubwa umeanguka na umekauka vizuri, ambao wenyeji wanaupenda sana kwa kutumia kwa vile kuni zake hazitoi moshi n.k. Sasa huyo mtema kuni akaanza kukata kuni na kurundika mzigo mkubwa tu. Jua lilipozidi kuwa kali jamaa akavua nguo akabaki uchi (hakutarajia mtu kutokea maeneo hayo kwa vile ni mbali na makazi ya watu) huku akiendelea na kupasua kuni toka kwenye lile gogo. Ikatokea jamaa akawa amechoka na pia jua kali, kwa hivyo akaamua kukaa juu ya lile gogo kupumzika. Sasa lile gogo lilikuwa lina ufa (kutokana na kutanuka kwa jua kali), kwa hivyo nyanya zikawa zimening'inia kwenye huo ufa. Baada ya kitambo kirefu kupita, jua nalo likawa linazama; kwa hivyo jamaa akaamua kunyanyuka ili ajitayarishe kuondoka. Sasa kumbe lile gogo lilikuwa limeshaanza ku-contract (kusinyaa); kwa hiyo nyanya zikashindwa kutoka. Jamaa wakati anakukuruka, huku contraction ya gogo inaendelea taratibu; jamaa akajikuta immediate options zimekauka kwa vile hakuweza kujinasua na shoka lilikuwa mbali hivyo hawezi kuzikata nyanya ili atoke. So, jamaa ndio akafia pale juu ya gogo baada ya mateso ya muda mrefu, kwani hata kelele alizopiga hazikuweza kusikika kijijini ambako palikuwa mbali. Kwa hivyo, ndugu, jamaa na marafiki walipomtafuta ndio wakamkuta jamaa amejifia juu ya gogo na nyanya zimenasa ndani ya gogo....! Kwa hivyo ikaonekana ni mateso makubwa mno mtu anayoweza kuyapata, so watu wakawa wanafanya reference kwamba ukifanya jambo baya/ukaidi n.k then utakiona cha mtema kuni

Mdau @X-PASTER yeye alitoa simulizi hii: Hii methali inatokana na hadithi au simulizi ya mkata kuni (Mtema kuni... Hiki ni kiswahili cha zamani). Kwa ufupi inasimuliwa kwamba mkata kuni alikwenda porini kwa nia ya kutema kuni (kukata kuni) kutokana na sababu anazo zijuwa yeye au kwa kuzidiwa na mawazo alipofika porini akapitiwa na usingizi (kama bado nakumbuka vizuri) ndio kwanza ulikuwa muda wa Mawio yaani jua linachomoza). Alipokurupuka... kuangaza huku na huku shoka halioni, na hali anakumbuka vizuri kulichukuwa... Yeye hakahisi labda limedondoka mahali... akaanza kulitafuta kuanzia Mawio mpaka Machweo (Kuzama kwa jua Wakati wa Magharibi) Mwisowe akajikuta amechoka na shoka halionekani. Akaamua kukaa chini ya mti ili apumzishe akili na kutafakari upya wapi alipolidondosha shoka lake. Wakati anajiandaa kukaa chini kuangalia begani kwake analiona shoka lake... kumbe alikuwa amesahau kuwa shoka lilikuwa amelining'iniza begani kwake... Hapo ndipo palipo patikana huo msemo wa "Utakiona cha mtema kuni... Kutafuta shoka wakati lipo begani."

Msemo huu umekuwa ukitumika na jamii ya wazungumza Kiswahili. Hata hivyo, umekuwa ukitumika kimazoea tu ikiwa ni kama kawaida ya jamii kurithi tamaduni pasi na kuuliza mzizi wake. Dira Leo tumejaribu kutafuta chanzo na asili ya msemo huu ili kuweza kufahamu kina na dhati yake. Pamoja na jitihada zetu, hatukufanikiwa kupata hakika hasa ya msemo huu kutokana na kutokuwepo na chanzo cha uhakika kuhusu msemo huu. Hata hivyo, tumepata baadhi ya hadithi zinazojaribu kueleza kuhusu msemo huu lakini hazijathibiti kama ndizo hakika ya msemo huu ama la.

Kwenye Jukwaa la JamiiForums, mwaka 2009, mdau mmoja @Mzizi wa Mbuyu alizua mada hii akijaribu kutafuta asili ya msemo huu. Wadau walipokea mjadala huu kwa kila mmoja kutoa alichonacho kuhusu huu msemo ikiwa ni sehemu ya masimulizi aliyosimuliwa au dhana alizosikia kwa watu. Kiujumla mjadala ulitiririka namna hii:

Mdau mwingine ni @Madam Koku: Mi huwa nafahamu simulizi tofauti kuhusu ''kukiona cha mtemakuni'', sikuwahi kusikia pia hizo zilipoelezwa hapo juu. Niliambiwa kuwa mtema kuni ni mtu anaekata kuni na alieenda kukata kuni porini na alipokuwa anataka kuzifunga kuni pamoja akawa anatafuta kamba, na bila kujua akamgusa nyoka akidhani ni kamba ili afungie kuni, loooo! kilichofuata ni mapambano... kwa hiyo hicho ndo kilikuwa ''cha mtemakuni'' nilichokifahamu. It is so intresting kuwa kuna simulizi tofauti tofauti kuhusiana na msemo uleule. Na nafikiri mambo kama haya yangehifadhiwa vizuri (yangekuwa well documented) ingesaidia kwa vizazi vijavyo hasa ukizingatia kiswahili kinakua sana sasa hivi ktk nch nyingi za Afrika.