
DIRA LEO
February 1, 2025 at 07:44 AM
Anasema walifanya kazi hiyo ya kuchosha na kutia hasira hasa wakizingatia kwamba haina malipo. Lakini kutokana na huko kutolipwa, walibuni njia ya kuwaletea pesa zaidi ya ile waliyotamani kulipwa.
Kwenye Ghala lile la mafuta, kulikuwa na sehemu yenye vitabu vya watoto vyenye soga za kuchekesha. Msimamizi wa ghala akawaabia kwamba kila siku vinaletwa vitabu vipya na wala hakuna matumizi kwa vitabu vile baada ya kuletwa pale.
Walipozungumza na baba yao, akawaruhusu wavitumie kwa wanachotaka kufanyia.
Waliporudi nyumbani, Kiyosaki na rafiki yake wakabuni maktaba ndogo ya kujisomea kwa watoto. Wakamchukua mdogo wao wakamuweka kama mfanyakazi wa maktaba ile na kumlipa dola tano kwa wiki.
Ikawa kusoma kwenye ile maktaba ni kati ya masaa matatu hadi matano na kwa tiketi yenye thamani ya dola moja. Wakaweza kutengeneza zaidi ya dola tano kwa siku. Wakaweza kumlipa mdogo wao na kumudu mahitaji yao ya msingi.
Kutokana na kufanya kazi bure, kukawafanya kutafuta njia ya kuingiza kipato zaidi.
Nahitimisha kwa kumnukuu tena Kiyosaki alipotoa maana ya tajiri kwamba, tutakupima kama wewe ni tajiri pale tukikutoa kwenye ajira yako, ni kiasi gani utahimili na kwa muda gani kumudu gharama zako za maisha ya kila siku.
Mwisho, Kiyosaki anasisitiza kuwekeza kwenye "Asset" na siyo "Liabilities" na kwake, nyumba ya kuishi ni "Liability" _Robert Kiyosaki (2012):Rich Dad Poor Dad.
👍
1