
DIRA LEO
February 1, 2025 at 03:00 PM
Tunapoangalia swala la maendeleo yatupaswa kuangalia Sekta ya Elimu ambayo ni miongoni mwa
Sekta za msingi zinazoleta maendeleo. Kwa kuona hilo ,Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania chini ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Leo tarehe 01 /02/2025 amezindua Sera ya 2014 Toleo la 2023,Elimu Na Ujuzi ndiyo mpango mzima.Ambayo inalenga Katika kuleta Mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu kutoka katika ufundishaji wa nadharia mpaka ufundishaji weka vitendo.
Sera hii itachagiza katika kumuwezesha Mwanafunzi kwendana na Ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia,itahakikisha upatikanaji wa Elimu bora utakao muwezesha mwanafunzi kujiamini na kwenda sambamba na soko la ajira.
Kwa kuhakikisha hilo Serikali imejenga na inaendelea kujenga na kukarabati vituo vya Elimu vitakavyo hakikisha Upatikanaji wa Elimu Bora nchini Tanzania.
Mabadiliko haya ya elimu yaweze kutupepea na sio kutupeperusha.Mabadiliko haya yawe yenye kuleta tija chanya kwa Watanzania .
👍
1