Prof. Hamadi Iddi Boga
February 22, 2025 at 09:34 AM
Leo asubuhi, nimehudhuria hafla katika Madrassa Azhar Kinango, ndani ya Wadi ya Kinango. Nimezungumza na wazazi, nikiwahimiza kuwalea watoto wao kwa maadili mema na kuwa makini katika malezi yao. Nilisisitiza kuwa kuwaacha watoto bila mwongozo kunawafanya waingie katika makundi hatari yanayotishia usalama wa jamii kwa vitendo vya uhalifu.
Miongoni mwa waliokuwepo ni Sheikh Faraj Omar, Sheikh Digo Dziro, Ustadh Ahmed, na viongozi wengineo.
👍
1