
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 16, 2025 at 05:52 AM
https://www.instagram.com/reel/DGH1qhnN_cL/?igsh=MW83N2h3ODZucGtwZQ==
*Delta Airlines kusherehekea Miaka 100 tangu kuanzishwa kwake, Ikiwa na ndege 986.*
Shirika la ndege la Delta Air Lines limeanza shamrashamra za sherehe za kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake kwa kuzindua ndege zake mbili mpya aina ya Airbus A350-900 (N527DN) na Airbus A321neo (N589DT).
Ndege ya A350-900 yenye namba ya usajili N527DN/MSN720, ambayo imepakwa rangi maalum ya maadhimisho ya miaka 100, imefanya majaribio yake ya kwanza ya injini katika Uwanja wa Ndege wa Airbus Toulouse, Ufaransa. A350-900 imepakwa rangi ya kipekee ambayo ni mchanganyiko wa rangi ya bluu na fedha, injini za bluu, na ncha za mabawa za bluu, ikiwa ni alama ya safari ndefu ya Delta katika kitoa huduma zake kwenye sekta ya anga.
Delta Air Lines ilianzishwa Machi 2, 1925, ikitambulika kama Huff Daland Dusters, Safari yake ya kwanza ya abiria ilifanyika Juni 17, 1929, ikiwa na jina jipya la Delta Air Service.
Kwa sasa, Delta ni moja ya mashirika makubwa zaidi ya ndege duniani ikiwa na jumla ya ndege 986 za aina mbalimbali zikiwemo ndege za Boeing 767, Airbus A330, Airbus A350, Airbus A321, Airbus A220, na Embraer ERJ-145.
Shirika hili linatoa huduma ya usafiri katika maeneo 275 duniani,yakiwemo maeneo ya Afrika na Mashariki ya Kati, Asia na India, Canada, visiwa vya Caribbean, America ya Kati na Kusini, na barani Ulaya.
Delta inatambulika kwa mtandao wake mkubwa ikiwa na jumla ya vituo 275 vya operesheni (hubs), kikiwemo kituo cha Amsterdam, Atlanta, Bogota, Boston, Detroit, Lima, London-Heathrow, Los Angeles, Mexico City, Minneapolis-St. Paul, New York-JFK na LaGuardia, Paris-Charles de Gaulle, Salt Lake City, Santiago (Chile), São Paulo, Seattle, Seoul-Incheon na Tokyo.
Taarifa kutoka Simple flying news zimeelezea kuwa, Delta Air Lines inashikilia nafasi ya pili miongoni mwa mashirika makubwa zaidi ya ndege duniani, nafasi ya kwanza ni ya shirika la ndege la United Airlines, huku Air China ikishika nafasi ya tatu.
.
#airlines #deltaairlines #100yearsanniversary