Aviation Tanzania 🇹🇿  WhatsApp Channel

Aviation Tanzania 🇹🇿

141 subscribers

About Aviation Tanzania 🇹🇿

A channel dedicated to aviation news and information from Tanzania and around the globe.

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/12/2025, 1:12:50 PM

https://www.instagram.com/p/DKzUSkwNDdj/?igsh=MTIwdWdyazllYTlkeQ== *Polisi Wathibitisha Hakuna Aliyenusurika Katika Ajali ya Ndege ya Air India.* Polisi nchini India wamethibitisha kuwa hakuna mtu aliyenusurika katika ajali ya ndege ya Air India aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyotokea mchana wa leo, dakika chache baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Ahmedabad kuelekea London. Kwa mujibu wa mamlaka za usalama, ndege hiyo ilianguka kwenye jengo la bweni la Chuo cha Tiba cha B.J., karibu na uwanja wa ndege, na kusababisha vifo vya wanafunzi kadhaa waliokuwa ndani ya bweni hilo wakati wa ajali. Maafisa wa polisi wamesema kuwa eneo la tukio tayari limesafishwa kwa asilimia 70 hadi 80, na juhudi za kuwaokoa waliokwama zinaendelea. Shirika la habari la CNN News-18 limeripoti kuwa, sehemu ya ndege hiyo iliangukia moja kwa moja kwenye eneo la chakula la wanafunzi, likionyesha picha za mabaki ya ndege juu ya paa la jengo na moshi mzito ukifuka angani. Ndege hiyo ilikuwa ikielekea Uwanja wa Ndege wa Gatwick, kusini mwa London, ikiwa na abiria 230 na wafanyakazi wa ndege 12 (ambao wote wamepoteza maisha). Kwa mujibu wa Air India, abiria hao ni pamoja na raia 169 wa India, 53 Waingereza, 7 kutoka Ureno, na mmoja kutoka Kanada. Watoto 11 na watoto wachanga wawili. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Flightradar24, ndege hiyo ilitengenezwa mwaka 2013 na kuanza kuhudumu rasmi katika shirika la Air India mwezi Januari 2014. Rais wa Uingereza Keir Starmer na Mfalme Charles wote wametuma salamu za rambirambi, huku serikali ya Uingereza ikieleza kuwa inashirikiana kwa karibu na India kufuatilia tukio hilo na kuwasaidia raia wake waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alieleza majonzi yake kupitia ukurasa wake wa X akieleza kuwa ajali hiyo ni ya kuhuzunisha na anaungana kwa pamoja na familia zote zilizoathirika katika kipindi cha maombolezo. Kampuni ya Boeing imethibitisha kuwa inafuatilia kwa karibu tukio hili na imeanza kushirikiana na mamlaka za India kuchunguza chanzo cha ajali. Hii ni ajali ya kwanza inayohusisha vifo kwa ndege ya aina ya Dreamliner tangu ianze kutumika mwaka 2011. #planecrash #airline #airindia #boeing787dreamliner #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/12/2025, 10:33:46 AM

https://www.instagram.com/reel/DKzCX1rN81f/?igsh=MXR0Mjh4a3phcjlkbA== *Ndege ya Air India yenye abiria 230+ yapata ajali* Ndege ya Air India aina ya Boeing 787-8 Dreamliner yenye namba ya usajili (VT-ANB) iliyokuwa ikielekea London Gatwick imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Ahmedabad, nchini India. Ndege hiyo ilikuwa ikifanya safari namba AI171, ikiwa na abiria 230 na wahudumu 12. Kwa sasa zoezi la Uokoaji wa manusura wa ajali hiyo linaendelea likifuatiwa na zoezi uchunguzi. Chanzo: @samchui #planecrash #airline #airindia #boeing787dreamliner #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/13/2025, 7:31:43 AM

https://www.instagram.com/p/DK1SCkONk7a/?igsh=MXhwNThieWV6bDF2dQ== The CEO of @fly.ethiopian , Mr.Mesfin Tasew Bekele, participates in a panel discussion on the development of Africa’s aviation sector during the AviaDev 2025 conference in Zanzibar. #Airlines #ethiopianairlines✈️ #aviadev #aviationcareer #aviadevafrica #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/13/2025, 6:07:58 AM

https://www.instagram.com/p/DK1IbDKttU8/?igsh=MXFiZG5rMjc0cGR3dA== *Abiria mmoja anusurika katika ajali ya Air India, asimulia hali ilivyokuwa** Wakati dunia ikiomboleza ajali mbaya ya ndege ya Air India iliyotokea mchana wa Alhamisi Juni 12,2025 na kusababisha vifo vya mamia ya watu waliokuwemo ndani ya ndege hiyo, taarifa mpya zimetolewa na kuvunja hali ya ukimya zinazothibitisha kuwa abiria mmoja pekee amepatikana hai. Vishwash Kumar Ramesh, raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 40, alipatikana akiwa hai katikati ya miili ya marehemu katika eneo la ajali, saa chache baada ya polisi kuthibitisha kuwa hakuna mtu aliyenusurika. Alikimbizwa Hospitali ya Serikali ya Asarwa, Ahmedabad, ambako kwa sasa amelazwa katika wodi ya kawaida, akiwa na majeraha ya kifua, macho na miguu. Vishwash alisimulia kuwa muda mfupi tu baada ya ndege hiyo kupaa, alisikia mlio mkubwa kisha ndege ikaanguka ghafla. Alisema tukio hilo lilitokea kwa kasi ya kushangaza kiasi kwamba hakuwa na muda wa kuelewa kilichotokea. Alipoamka, alijikuta akiwa katikati ya miili ya watu waliopoteza maisha. Alieleza kuwa alikuwa na hofu kubwa na alipoona anaweza kusimama, alikimbia kutoka eneo hilo huku akizungukwa na mabaki ya ndege. Mtu mmoja alimtokea na kumsaidia kumpakia kwenye ambulensi, na ndipo akafikishwa hospitalini. Ndege hiyo aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, iliyokuwa ikielekea Uwanja wa Ndege wa Gatwick, Uingereza, ilibeba watu 242 wakiwemo wafanyakazi wa ndege. Air India imethibitisha kuwa kati ya abiria 230, 169 walikuwa raia wa India, 53 Waingereza, 7 kutoka Ureno, na 1 kutoka Kanada. Vishwash alikuwa akirejea London pamoja na kaka yake, Ajay Kumar Ramesh, mwenye umri wa miaka 45, baada ya kutembelea familia yao nchini India. Alieleza kuwa yeye na kaka yake walikuwa wametoka kutembelea mji wa Diu, lakini walikuwa wamekaa katika mistari tofauti ndani ya ndege. Aliongeza kuwa hadi sasa hajui aliko kaka yake na anaendelea kumtafuta, akitumai bado yuko hai. Katika hospitali hiyo hiyo, mamia ya ndugu na jamaa wa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo wanaendelea kufuatilia taarifa, huku wengine wakitafuta wapendwa wao ambao bado hawajapatikana. Taarifa hizi zimetolewa baada ya Kamishna wa Polisi wa Ahmedabad, G.S. Malik, awali kusema kuwa hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo, kutokana na mlipuko mkubwa ulioharibu kabisa sehemu ya ndege na kusababisha vifo vingi papo hapo, wakiwemo wanafunzi waliokuwa kwenye bweni la Chuo Kikuu cha Tiba cha B.J. ambako ndege hiyo iliangukia.

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/11/2025, 7:18:13 AM

https://www.instagram.com/reel/DKwGwSJNs21/?igsh=MzhvcnNoMzhmOHpp *Mwanamke mrefu zaidi duniani hulazimika kulipia Siti 6 kila anaposafiri kwa ndege* Wakati abiria wengi wanaotumia usafiri wa anga hutumia siti moja pekee kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine, hii ni tofauti kwa Rumeysa Gelgi, raia wa Uturuki ambaye anavunja rekodi ya dunia (Guinness World Records) kwa kuwa mwanamke mrefu zaidi duniani. Rumeysa Gelgi, ambaye ana urefu wa futi 7 na inchi 0.7 (sawa na mita 2.15), amefichua kuwa kila anaposafiri kwa ndege hulazimika kulipia siti sita kutokana na hali yake ya kiafya inayomlazimu kulala kwenye machela wakati wote wa safari. Gelgi, ambaye anaishi katika jimbo la Karabük, kaskazini mwa Uturuki, anasumbuliwa na ugonjwa nadra unaojulikana kama Weaver syndrome, hali inayosababisha ukuaji wa haraka wa mwili pamoja na changamoto nyingine za kiafya. Kwa sababu ya urefu wake wa kipekee, amekuwa akitegemea kiti cha magurudumu. Kwa miaka mingi, alikuwa hawezi kabisa kusafiri kwa ndege kutokana na kutokuwepo kwa nafasi ya kutosha. Lakini kupitia Shirika la Ndege la Turkish Airlines, sasa anaweza kusafiri kimataifa baada ya shirika hilo kuondoa siti sita katika ndege moja na kuweka machela maalum kwa ajili yake. Safari yake ya kwanza ya anga ilifanyika mwezi Septemba mwaka 2022 kutoka San Francisco hadi Istanbul. Aliielezea safari hiyo kama “safari kamili na isiyo na dosari.” Tangu wakati huo, Rumeysa amekuwa akisafiri angalau mara moja kila mwaka, lakini ni kwa kutumia shirika lake la taifa pekee, ambalo lina uwezo wa kutoa huduma hiyo maalum. Licha ya kuwa tayari ametembelea mataifa kama Marekani, Uingereza, Hispania na Italia, kila safari huambatana na maandalizi makubwa na gharama kubwa. Mbali na kulipia nafasi ya machela ambayo ni sawa na siti sita za abiria wengine, anahitajika kufika uwanja wa ndege saa nne kabla ya muda wa safari kwa ajili ya kukutana na wataalamu wa afya na maandalizi mengine ya usalama. Hadi sasa, hajawahi kusafiri kwa basi au treni, lakini ana matumaini ya kufanya hivyo katika miezi ijayo. Katika mahojiano na Luxury Travel Daily, Rumeysa alieleza jinsi anavyoumizwa na hali ya kushindwa kutembelea maeneo yenye historia ya kuvutia kutokana na ukosefu wa njia salama. Kutokana na uwepo wa vyuma vya msaada mgongoni mwake, hata kuanguka kidogo inaweza kuwa hatari kubwa kwake. Gelgi anapanga kutembelea miji mashuhuri ya Asia Mashariki kama Tokyo, Kyoto, Shanghai na Seoul. Lakini ndoto yake kubwa zaidi ni kutembelea mji wake wa asili, Safranbolu, hasa maeneo ya kihistoria kama “Old Town” yanayojulikana kwa majumba ya Kiosmani yaliyoifadhiwa vyema. #worldtallestwoman #guinnesworldrecord #turkishairlines #flywithturkishairlines #passengerseat #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/13/2025, 6:09:23 AM

https://www.instagram.com/reel/DKzuwGFNhbb/?igsh=MXFpNmgydWtyMXJnaA== Katika Mkutano wa Kimaendeleo ya sekta ya anga,Aviadev ,Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la ndege la @airtanzania_atcl Mhandisi Peter Ulanga ameeleza mipango ya hivi karibuni ya shirika hilo ikiwemo kuanzisha safari katika visiwa vya Pemba. #airline #airtanzania #routeexpansion #newaircraft #airtanzania_atcl #aviation #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/13/2025, 10:18:08 AM

https://www.instagram.com/p/DK1lkv7taQF/?igsh=M2Q5dWJoZDI1Yzg4 *”Blackbox” ya ndege ya Air India yapatikana katika eneo la ajali* Mamlaka za India zimethibitisha kupatikana kwa moja kati ya vifaa viwili vya kurekodi taarifa muhimu (black box) kutoka kwenye ndege ya Air India safari namba AI171, ambayo ilianguka muda mfupi baada ya kuanza kupaa siku ya Jana juni 12,2025. Taarifa kutoka chombo cha habari cha Hindustan Times zinaeleza kuwa kifaa hicho kilipatikana asubuhi ya Leo, ingawa bado haijafahamika kama ni kifaa cha kurekodi mazungumzo ya marubani (Cockpit Voice Recorder) au taarifa za kiufundi za ndege (Flight Data Recorder). Kifaa hicho kinatarajiwa kutoa mwanga kuhusu dakika za mwisho kabla ya ajali hiyo mbaya kutokea. Wachunguzi sasa wameanza kuchambua mabaki ya ndege hiyo aina ya Boeing Dreamliner katika juhudi za kubaini chanzo cha ajali iliyosababisha vifo vya watu 241 kati ya 242 waliokuwemo, na kuifanya kuwa ajali ya anga mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja. Kwa sasa, chanzo halisi cha ajali hiyo hakijafahamika. Hata hivyo, wataalamu wa usalama wa anga wana matumaini kuwa uchambuzi wa black box hiyo utatoa taarifa muhimu zitakazosaidia kueleza kilichojiri ndani ya dakika chache baada ya ndege hiyo kupaa. Ripoti ya awali ya uchunguzi inatarajiwa kutolewa ndani ya siku chache zijazo. #planecrash #blackbox #planecrashinvestigation #airindia #boeing787dreamliner #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/13/2025, 8:56:50 AM

https://youtu.be/kHOxaxJIKhI?si=2fVD_ZkvhMfNIUWf

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/12/2025, 9:28:23 AM

https://www.instagram.com/p/DKy67lktNC1/?igsh=MWZ2dWUyeTJoYWRpcQ== *Mashirika ya Ndege 46 na Wajumbe 500 Wakutana Katika Mkutano wa Maendeleo ya Sekta ya Anga Zanzibar.* Zaidi ya mashirika ya ndege 46 na wajumbe 500 kutoka mataifa mbalimbali duniani wamekutana visiwani Zanzibar kushiriki Mkutano wa Maendeleo ya Sekta ya Anga Afrika (AviaDev Africa), unaofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip. Mkutano huu umezinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni mgeni rasmi wa tukio hilo ukiwakutanisha Wakurugenzi Wakuu wa mashirika ya ndege, viongozi wa viwanja vya ndege, maafisa wa bodi za utalii, na wawakilishi wa serikali kutoka Afrika na kwingineko duniani. Mkutano huo umetajwa kusaidia ongezeko la safari za moja kwa moja visiwani Zanzibar na maeneo mengine ya Afrika kwa njia ya ushirikiano wa kimkakati kati ya sekta binafsi na serikali, ili kuchochea ukuaji wa utalii na uchumi wa ndani. Mkutano huo unajumuisha majadiliano ya ana kwa ana baina ya mashirika ya ndege na viwanja vya ndege, mijadala ya kitaalamu kuhusu usafiri wa anga, pamoja na maonyesho ya fursa za uwekezaji. #aviadev #aviation #aviationprofessionals #aviationenthusiast #aviationtanzania✈ #aviatamedia

Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
6/10/2025, 6:33:45 PM

https://www.instagram.com/p/DKuu_o1tuFY/?igsh=bWw3ZXN5ampsMnB2 *Zanzibar yapiga hatua mpya kuelekea kuanzisha Shirika la ndege la Kitaifa.* Zanzibar iko katika mazungumzo na wawekezaji mbalimbali kuhusu mpango wa kuanzisha shirika lake la ndege la kitaifa hatua inayolenga kuboresha muunganiko wa visiwa hivyo na kukuza sekta ya utalii. Tangazo hilo lilitolewa Jumatatu katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichofanyika Chukwani, ambapo Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mheshimiwa Nadir Abdulatif Yussuf, alieleza kuwa serikali ya Zanzibar tayari iko katika mazungumzo na shirika la ndege la EgyptAir kuhusu mpango wa kushirikiana kuanzisha shirika hilo jipya. Mheshimiwa Yussuf alibainisha kuwa majadiliano na EgyptAir yanaendelea vizuri, na kwamba pande zote mbili tayari zimefikia makubaliano ya awali ya kuweka mfumo wa ushirikiano kwa ajili ya kuanzisha shirika la ndege la Zanzibar. Kauli hiyo imetolewa kufuatia hoja iliyotolewa na Mwakilishi wa Mtambwe, Dkt. Mohamed Ali Suleiman, ambaye aliitaka serikali kuangalia kama huu ndio wakati muafaka wa kutekeleza mpango wa muda mrefu wa kuwa na shirika la ndege litakalotambulika kitaifa kutoka Zanzibar. Ikiwa mpango huu utakamilika, utaiweka Zanzibar katika nafasi nzuri ya kushindana kikanda katika sekta ya usafiri wa anga, huku ukitarajiwa pia kuongeza idadi ya watalii wanaofika visiwani kwa urahisi zaidi. Chanzo: The Citizen #Airlines #zanzibar #newairline #aviationcareer #aakia #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Link copied to clipboard!