Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 17, 2025 at 08:33 AM
https://www.instagram.com/p/DGKtI0ntSO5/?igsh=ZW42bnFvY2Y1NW83 *Paul Meyer: Fundi aliyeiba ndege ya jeshi ili arudi nyumbani kumuona mke wake.* Paul Meyer,aliyekuwa Sajenti wa Jeshi la Anga nchini Marekani, Mei 23, 1969 alifanya jaribio la hatari la kurejea nyumbani kumuona mke wake huko Virginia. Meyer, ambaye alikuwa msaidizi wa mkuu wa kituo cha matengenezo ya ndege cha RAF Mildenhall, kilicgopo Uingereza, alitarajiwa kurejea nyumbani baada ya mwezi mmoja,lakini alishindwa kungojea mwezi mmoja kutimia ndipo alipoamua kufanya maamuzi yaliyowashangaza wengi. Baada ya kulewa kupindukia usiku mmoja kesho yake asubuhi alifanya hila kwa wasimamizi na kuwadanganya kuwa yeye ni afisa wa cheo cha juu, kisha akafanikiwa kuipata ndege ya kijeshi aina ya Lockheed C-130E Hercules, na kuondoka nayo kwa mwendo wa kasi bila idhini yoyote. Mpango wake ulikuwa wa hatari lakini ulitawaliwa na hisia kali, alipanga kuruka peke yake na kuvuka Bahari ya Atlantiki ili afanikiwe kumuona mke wake. Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuruka, hali ikawa mbaya. Katika mawasiliano yake ya mwisho na mke wake kupitia redio, Meyer alisikika akitoa maneno haya yaliyotia hofu: "Niacheni kwa takribani dakika tano, nina matatizo." Takriban saa mbili baada ya safari yake kuanza, ndege hiyo ilipotea kwenye rada na baadaye ikaanguka baharini karibu na Kisiwa cha Alderney. Baadhi ya mabaki ya ndege yalipatikana wakati huo, lakini mwili wa Meyer haukupatikana kamwe. Jaribio lake la kusikitisha likawa fumbo lililodumu kwa miongo mingi. Takriban miaka 50 baadaye, timu ya wachunguzi wa majini kutoka Uingereza, inayojulikana kama Deeper Dorset, ilianzisha msako wa kuitafuta ndege hiyo iliyopotea. Kupitia kampeni ya kuchangisha fedha mtandaoni iliyokusanya dola 8,000, walichunguza eneo la maili 10 za mraba chini ya bahari kwa siku 20. Hatimaye, katika siku ya mwisho ya utafutaji wao, kifaa cha sonar kiligundua kitu kinachofanana na mabaki ya ndege kubwa katika eneo sahihi. Ingawa hali mbaya ya hewa ilichelewesha uchunguzi zaidi, uchambuzi wa awali wa data ya sonar ulidokeza kuwa mabaki hayo huenda yakawa ya ndege ya Meyer. Timu ya Deeper Dorset ilipanga kurejea na vifaa maalum vya upigaji picha chini ya maji ili kuunda mfano wa sehemu ya ajali, jambo ambalo lingeweza kufichua sababu halisi za kuanguka kwa ndege hiyo. Ugunduzi huu uliibua hisia mseto kwa familia ya Meyer, huku baadhi yao wakihisi huzuni, na wengine kupata tumaini kwamba hatimaye wangepata majibu ya kile kilichotokea siku ya ajali mwaka 1969.

Comments