
DAWA ZA ASILI
February 18, 2025 at 12:25 PM
SIDA ACUTA NI MMEA WA DAWA WENYE NGUVU ZA ASILI ZA MIUJIZA PAMOJA NA UWEZO WA UPONYAJI WA MAGONJWA.
Mmea wa dawa wa Sida acuta ni mmea wa familia ya malvaceae ambao unastawi kwenye nchi za hali ya hewa ya tropic na ikweta.
UWEZO WA SIDA ACUTA KUPONYESHA MAGONJWA.
Mmea wa dawa wa Sida acuta ni mmea wenye uwezo wa kuponyesha magonjwa ya kuharisha, kiungulio na kuvimbiwa kwa chakula kisichosagwa tumboni.
Pia mchemsho wa majani ya mmea huu wa Sida acuta hutumika kuogea ili kutibu miwasho ya mwili mbalimbali.
UWEZO WA SIDA ACUTA KWENYE NGUVU ZA ASILI ZA MIUJIZA.
Kwa kiasi kikubwa umaarufu wa mmea huu upo kwenye matokeo ya uratibu wa matumizi yake ya nguvu zake za asili za miujiza.
Nitaongelea ule uwezo wake ambao haukiuki sheria za hadhara juu ya siri zisizotakiwa kuelimishwa hadharani.
Tawi ndogo lenye majani machache hutumika kupata maono ya matukio ya mbele kwa kuliweka tawi hilo ndani ya mto kisha usiku mto hutumika kama kawaida ambapo mtumiaji utakapo lalia atapata maoni ya matukio yote ya muda ujao kwa njia ya ndoto. Kama hatapa maono hayo anashauriwa kuushirikisha na mmea mwingine uitwao Nerium africana kwa kufuata kutimiza masharti yale yale.
Kihistoria makabila mengi ya kiafrika wanaufahamu mmea huu kwa kazi yake ya kufukuza balaa na laana.
Kutokana nguvu yake ya kufukuza balaa na laana makabila mengi yaliuchagua mmea huu utumike kama fagio ili wakati wa kufagia uchafu kwenye makazi uweze pia kufagia takataka za nguvu za giza za laana, mikosi na mabalaa kwenye makazi ya nyumba zao. Na kwa kiasi kikubwa inasemekana kulikuwa na matokeo makubwa yaliyo chanya.
Pia mmea huu ulitumika kulaani watoto bila wao wenyewe kujua kwa njia ya kuwapiga watoto hao kwa kutumia fimbo ya mmea huo. Inasemekana wengi waliopigwa kwa kutumia fimbo ya mmea huo walipata matatizo makuwa kwenye maisha yao ambayo yalihitaji msaada wa kuwanasua kwenye shida hizo
Tatizo la kijamii ni pale waliojuwa uwezo wa nguvu za asili miujiza za mmea huu kutoelimisha wengine kuhusu sababu za