
DAWA ZA ASILI
March 1, 2025 at 08:40 AM
Unaitwa Mnyaa kitaalamu unaitwa Petroleum Plant na katika majina ya kibotanika unaitwa Euphorbia Tirucalli na wengine pia huuita PENCIL TREE
Shuka na uzi huu ufahamu unatibu nini na unatumikaje
Unaondoa sunzua
Pia Yale maziwa yake ni gundi safi sana Kwa kugundisha karatasi
Huu mmea kwa watoto wa kiume wakiona hawajatahiriwa umri unaenda wanajiwekea maziwa ya huu mmea kwenye uume, inawavimbisha . Mzazi anampeleka kumtahiri
Hii ni dawa sana kwa mtu aliyewekewa sumu kwenye chakula. Mtu akipewa sumu au ulozi kwenye chakula, unachukua maziwa kama nusu Lita hivi, halafu unachanganya na maziwa maziwa ya mti huu wa mnyaa, halafu unakoroga mpaka ichanganyike vizuri, baadaye unampa huyo aliyelishwa sumu anakunywa yote.
Atatapika sumu yote.
Pia huo utomvu wake unakata viupele sugu mwilini Kuna vitu viota mwilini kama viupele kwetu tunaiea (sundo) kwa hiyo unakata kakipande kaßogo kanakoeoa utomvu basi ule utomvu unazungushia kale kaupelle sundo Kila siku utaona kanavyo kleki mwisho kanakateika
visundo ni aina furani ya upele mgumu ambao mara nyingi huota kwenye vidole vya mkona na rangi yake huwa nyeusi ila hakina maumivu hata unapokikata sasa kama unacho kwa kidole we kikate kwa wembe au kisu kikari ikitoka damu ni vizuri zaidi harafu unadondoshea utomvu wake,note nimesema kwa maeneo ya kiganja cha mkono
ni dawa kubwa sana kukinga bomba ni kiboko unachuna katawi Moja unaeka kwa nyumba juyamlango
Inasaidia kikohozi unakata kijiti halafu choma kwa moto kiyasi maziwa yake iwe maji tafuna ukimeza maji peke jion asubuhi uhakikishe isipowesana sana kwa watoto ikosawa sana
Pia ukichanganya na katanichanga, unatwanga pamoja unaloweka majikiasi nichanjo ya kideri
Linatibu maskio,kama linauma sasa,China kimoja,ueke ndani ya moto,dakika chache,hio maziwa lake litageuka maji,,utoe kwa moto uifinye kwa maskio hio maji lake lidondoke ndani ya maskio Mara 3.ufanye hivyo twais in a day
Hata majimaji yake ni dawa ya utomvu wake.utomvu wake ukiingia machoni unachukua sehemu yake unafikicha maji yakitoka unaweka kwenye jicho mtu anapona.
Na yanaleta maziwa ya mtoto kwa waliojifungua wakakosa maziwa
Zingatia mnyaa uko wa aina 2 wenye mti mdogo na mti mkubwa sana unatumia mti huo mdogo unachemsha majan yake unachanganya na togwa unakunywa
Kama umehisi kula au kunywa sumu cukuwa mayayi mawili yapasuwe weka matonya mawili tu canganya kisha pika ukimaliza kula sumu itatoka
Tahadhari usitumiye dawa hii ukiwa safarini maake ukiyutumia unaenda coo mara kwamara
Pia ni dawa ya .mashilingi sugu hayo maziwa yake unayapaka kwenye Hilo shilingi siku moja tuu usirudie inamaliza kabisa,
Ni dawa ya kikohozi pia unaubabua kwenye moto unatafuna nachumvi ladha inakuwa kama limao
Nikiwa kama mzee ambaye bado nipo hai niwape elimu mojawapo juu ya mti huu. Ukichomwa na miba ukavunjikia ndani ya mwili wako basi toboa tundu kidogo kama unauchomoa vile alafu paka utomvu huo ulale, kesho utaukuta karibu au nje kabisa
Ni dawa nzuri ya kuku Aina zote.inatibu kideri kmafua nk Unachuma then unapondaponda kidogo alafu unachanganya na maji kuku watakunywa kama maji lkn ni dawa
Dawa yake ni ndogo sana kama umendokewa huo utomvu wa mnyaa kwenye macho.
Mrumbasi naamini wengi tunaujua, chukua mbegu za mrumbasi weka kwenye jicho lililoingiwa na utomvu huo, huwa ni vimbegu vidogo sana kama punje ya haradali weka kwenye macho/ jicho lililopata shida , lala ha saa moja au mawili , ukiamuka awepo mtu wa kukutoa hizo mbegu, mbegu zote utaziona zimekusanya utovu wote, na huwa zina rangi nyeusi ila wakati huo zote zitakuwa nyeupe na zipo kwenye kope zimekusanya utomvu wote, ndio tayari umepona.
Ikindondokea jicho, unachoma tawi lake changa kwa jivu ikipoa unaweka majimaji YAKE kwa jicho na utapona Mara hiyo hiyo. Sio lazima maziwa ya mama.
Maziwa yake ukidondoshea kwenye uji wa ulezi au wa mtaama ni dawa nzuli kama ulipewa sumu
gundi nzuri hiyo kwa kuungia hela iliyo chanika
Utupa huo tunaitaga ivo ss watu ww pwani tunatumia huu kulewesha samaki kwenye mpango mara nyingi... Samaki lazima aje juu hoi kalewa
Kuna mmea mdogo kwa kisuma unaitwa ILUMBA huu mmea una mbegu nyeusi chambua vzr hizo mbegu endapo utakuwa utomvu wa mnyaa umeingia machoni weka hizo mbegu ndani ya jicho dk 5 nyingi utomvu wote utakuwa umekusanywa
Pia inatibu mtu aliyepatwa na shida ya miguu kufa ganzi .matumizi chukua mnyaa pondaponda afu changanya na mafuta ya taa afu jikandekande sehm ya mwili iliyopata ganzi inatibu haraka sana
Kama jipu ndo linaanza paka utomvu wake eneo la jipu, kesho linakuwa tayari kwaajili ya kukamuliwa
Huumti ukiuchukua kijiti chake jualikiwa halijatoka au limezama kiweke chini ya mlango wako sema maneno haya mkewangu akitoka njena mwanaume mwingine umewake usisimame hata akimuingiza hapandani isisi mame hapo kwisha napiya mwana mke akikuekea wewe mwanaume piya haisimami hataufanyeje ila tahazali uweke ukiwa wewe upo ndani usitoke hadiyeye atoke au kama yupo nje weka halafu muite ndani teali kauchukua ilawewe mwenjee ukipiga safi
NB ni dawa nziru sana ya visunzua unavikata kidogo na wembe ukaona damu inatoka weka huo utomvu wake Mara Moja tu Wala sio dose ya wiki kwisha habari yake
Pia wazee wako wakichelewa kukupeleka jando, dondoshea maziwa yake kwenye uume, fasta utapelekwa kutahiriwa
N.B: Linda sana macho yako! Maziwaziwa yake yale meupe yakidondokea usoni yanaweza kusababisha upofu .Mara ikitokea yakadondokea usoni mtafute haraka mama anayenyonyesha akuweke maziwa yake mara 2 hadi mara kwa siku unaweza pona
Wazee wetu ni hazina kubwa TUSIWAPUUZE bahati mbaya wengi wanakufa na ujuzi wao wa tiba asilia.
Asanteni