
Wizara ya Ardhi
February 4, 2025 at 06:27 PM
MWENYEKITI wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe Timotheo Mzava ameongoza kikao cha kamati hiyo chenye lengo la kujadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana, Makatibu Wakuu na Wataalamu wa Wizara hizo.
❤️
1