Wizara ya Ardhi WhatsApp Channel

Wizara ya Ardhi

231 subscribers

About Wizara ya Ardhi

Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi youtu.be/ciM4397iXWw?si=Fnl9uAKTWaiiIsOx

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/14/2025, 11:13:22 AM
Image
Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/13/2025, 5:56:34 PM

WASIOLIPA KODI NA KUENDELEZA MAENEO YA ARDHI WAANZA KUBANWA DSM Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza kuwabana wamiliki wote wa ardhi wasiolipa kodi ya pango la ardhi sambamba na kutoendeleza maeneo wanayomiliki. Wakiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa sharti la kulipa kodi na kuendeleza kwa wamiliki wa ardhi Mkoa wa Pwani tarehe 13 februari 2025, timu maalum ya ukaguzi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Mandeleo ya Makazi imesema hatua hiyo ni juhudi za wizara kukusanya kodi pamoja na kuhakikisha maeneo yanayomilikiwa na wananchi yanaendelezwa. Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mapato na Uwekezaji Wizara ya Ardhi Bw. Leonard Msafiri amesema, kwa mujibu wa sheria wamiliki wa ardhi wanatakiwa kulipa kodi ya pango la ardhi na wasipofanya hivyo wanapaswa kupewa notisi ya kulipa ndani ya siku kumi na nne. ‘’Ulipaji wa kodi ya ardhi ni wajibu wa kisheria kwa mmiliki chini ya fungu 33 la sheria ya ardhi sura 113’’. Amesema Akiwa katika shamba namba 57, 58, 59 na 60 lilipo Miswe Kibaha Mkoani Pwani, Kamishna wa Ardhi Msaidiźi Mapato na Uwekezaji Wizara ya Ardhi amemweleza mmiliki wa mashamba hayo kuwa ana nafasi ndani ya siku kumi na nne kulipa kodi ya ardhi. Aidha, Kamishna wa ardhi Msaidizi Mkoa wa Pwani Ndg. Hussein Sadiki Iddi, ameeleza kuwa ndani ya siku hizo kumi na nne mmiliki anaweza kufika Ofisi za ardhi ili kupewa ushauri na kueweka namna nzuri ya kufanya mazungumzo ya kulipa deni linalomkabili. Timu ya ukaguzi ilitembelea pia shamba namba 2 eneo la Miswe kata Mbwawa, halmashauri ya manispaa Kibaha ambapo mmiliki wake anadaiwa kiasi cha Tsh mil 690. Katika eneo hilo Kamishna Msafiri alielekeza mmiliki wake kupatiwa barua ya onyo ikiwa ni hatua ya kwanza ya mchakato wa ufutaji ardhi kwa mujibu wa fungu la 45 ya sheria ya ardhi sura ya 113. Barua hiyo alikabidhiwa Bw. Dunia Mrisho Kinyogoli ambaye ni mwakilishi Miswe Vile vile, timu hiyo ilitembelea kituo cha mafuta cha ATN picha ya ndege mkoani Pwani ambapo mmiliki wake amadaiwa kiasi cha Tsh 24. Mmiliki huyo alikabidhiwa barua ya onyo kupitia Meneja wa kituo Bw. Abdallah Bawazir. Kamishna Msafiri alieleza kuwa zoezi la kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi ni endelevu na linafanyika katika mikoa yote hivyo amehimiza wadaiwa wote wa kodi ya pango la ardhi kuhakikisha wanalipa madeni yao ili kuepuka usumbufu unaoweza kuwapata wakati wa kuendesha shughuli zao. --------------mwisho-------

Image
Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/14/2025, 11:14:50 AM
Video
Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/14/2025, 11:13:23 AM
Image
Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/12/2025, 10:09:01 AM

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Silo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Mhe Ummy Nderiyananga bungeni jijini Dodoma leo.

😊 1
Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/14/2025, 11:13:24 AM
Image
Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/15/2025, 9:21:24 AM
Image
Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/15/2025, 9:21:04 AM

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na wataalamu wa Ardhi wa Mikoa ya Dodoma na Manyara leo tarehe 19 Februari 2025 katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto.

Image
Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/12/2025, 6:43:04 PM

MAWAKALA SEKTA YA MIILKI WATAKIWA KUJISAJILI ARUSHA Mawakala wa Milki nchini wametakiwa kujisajili katika mfumo wa Wizara ya Ardhi ili kuingia kwenye mfumo rasmi utakaowezesha kutambulika. Hayo yameelezwa leo tarehe 12 Februari 2025 na Mratibu wa Mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa Wadau wa Sekta ya Milki Bi. Nuru Kimbe, mjadala uliofanyika mkoani Arusha. Amesema, ni vizuri mawakala wa milki wakajisajili katika mfumo ili waweze kutambulika katika kipindi hiki ambacho wizara inategemea kuwa na sheria ya milki. "Nasisitiza mawakala waweze kujisajili na waweke ‘details’ za masingi kama anuani na mahali wanapofanyia kazi". Amesema Bi. Nuru Kwa mujibu wa Bi. Kimbe ambaye ni Afisa kutoka Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, faida za kujisajili ni pamoja na kutambulika na serikali kitu alichokieleza kitarahisisha kazi kwa mawakala ambapo amesema hatua hiyo itarahisisha katika kazi zao kama wakala na kuwafikia wateja sambamba na kuaminika zaidi. Amebainisha kuwa, kwa sasa mijadala inafanyika kwenye majiji ambako soko la milki linafanyika sana na kuitaja majiji hayo kuwa ni Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na Mwanza. Hata hivyo, amesema wako katika mchakato wa kufika mikoa mingine inayokuwa sana katika soko la milki kama vile Tanga, Morogoro, Pwani na Mbeya huku nia ikiwa ni kufika nchi nzima. Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa kikao hicho kutoka kampuni ya GimcoAfrika Ltd Bw. Herien Muro amesema, elimu waliyopata kupitia kikao kazj ni muhimu kwa kuwa inaenda kuondoa udanganyifu huku ikiisaidia serikali kupata mapato. Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia kitengo cha Milki (REAL ESTATE) inaendesha mijadala ya pamoja na wadau kwa lengo la kupata maoni kuhusu utambuzi na usajili wa wadau wa sekta ya milki ili kuboresha na kukuza sekta ya milki nchini. ‐----‐--------mwisho-----

Video
Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
2/12/2025, 10:08:39 AM
Image
Link copied to clipboard!